Ni wazi kuwa kila toleo la program endeshi linapotoka kunakuwa na baadhi ya simu janja ambazo zimechakuguliwa kupata toleo hilo, Motorola nao waongeza idadi ya simu katika Android 13.
Motorola ni moja kati ya makampuni makubwa sana na ni kongwe ukilinganisha na makampuni mengi ya kutengeneza na kuuza simu na imeweka wazi matoleo yake ya simu ambayo yanakuja na Android 13.
Kwa mara ya kwanza kabisa kampuni ya Motorola ilitoa orodha ya simu zake ambazo zitapata toleo la Android 13 na kwa kipindi hicho ilikua ni matoleo ya simu 10 tuu.
Kwa saa kizuri ni kwamba kampuni imeongeza tena matoleo mengine 10 hivyo jumla yanakua ni matoleo 20.
Matoleo (Kwa Ujumla) Hayo Ni:
- Motorola Razr (2022)
- Motorola Edge 30 Ultra
- Motorola Edge 30 Pro
- Motorola Edge Plus (2022)
- Motorola Edge 30 Fusion
- Motorola Edge 30 Neo
- Motorola Edge 30
- Motorola Edge (2022)
- Motorola Edge 20 Pro
- Motorola Edge 20
- Motorola Edge (2021)
- Motorola Edge 20 Lite
- Moto G Stylus 5G (2022)
- Moto G 5G
- Moto G82 5G
- Moto G72
- Moto G62 5G
- Moto G52
- Moto G42
- Moto G32
Ukichana na habari hii kauchiwa lakini bado haijulikani kwamba ni lini baadhi ya vifaa vitatoka au ni lini vifaa hivyo vikapata toleo hilo la Android.
Mpaka sasa kuna baadhi ya matoleo kutoka Motorola ambayo yametoka hivi karibuni na hayajapata toleo la Android 13 mfano mzuri nit oleo la Moto G22 na Hata yale ya Muendelezo Wa Moto E.
Ni matoleo mengi ya simu Ambayo yanatumia Android kuwa na kiu ya kutumia Android 13 kwa vifaa ambavyo vinaruhusu ndio maana hata simu nyingi za juu zinavyotoka zinahakikisha zinaendana na toleo hilo kwa sasa
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment. Je hii umeipokeaje? Je ushawahi kutumia toleo la Motorola? Pata picha likipata pragramu endeshi ya Android13.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.