fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Android Apple Mtandao Usalama

Vijue Virusi vya Kompyuta na Simu Kiundani

Vijue Virusi vya Kompyuta na Simu Kiundani

Spread the love

Virusi vya kompyuta ni programu kama programu nyingine za kompyuta. Utofauti ni kwamba virusi vinafanya vitu amabavyo havitegemewi na mtumiaji na vina uwezo wa kujizalisha kwenye kompyuta, kitumi kingine au mtandao mzima. Virusi huweza kujizalisha na kujiamabatanisha na programu zingine, mafaili ya kompyuta na yale ya kawaida ya mtumiaji na hata sehemu ambapo kompyuta huanza kuwaka (‘boot sector’).

Virusi vya kompyuta hutengenezwa na watu wa rika mbalimbali, kuanzia vijana wadogo hadi watu wazima, ili mradi tu wanaijua lugha ya kompyuta. Watu hawa, almaarufu kama ‘maprograma’ hutengeneza programu hizo wakiwa na nia tofauti, zikiwemo za kibanfsi, za kisiasa na hata kibiashara. Virusi huweza kutengenezwa kulenga kompyuta ya aina yoyote. Kwa sasa, maprograma wengi wanalenga kompyuta zitumiazo mifumo ya ‘Windows’ na simu zitumiazo mifumo ya ‘Android’. Jambo hili ni sababu kuu inayowafanya kampuni ya ‘Apple’ na mifumo ya ‘Linux’ (kama ‘Ubuntu’) kutamba kwamba mifumo yao haina virusi, jambo amabalo si ukweli halisi. Ukweli ni kwamba zaidi ya asilimia 80 ya soko la kompyuta duniani hutumia mifumo ya Windows na sehemu kubwa ya soko la simu-janja (‘smartphone’) duniani hutumia Android. Hili linawavutia zaidi maprograma kutengeneza programu kwa mifumo hii zikiwemo virusi. Sababu nyingine kuu ni mashauri mblaimbali yaliyofanyika na mifumo hii ili kurahisisha utumikaji ilihari ikipunguza usalama wa mifumo hiyo.

SOMA PIA  Mfuko unaoweza kutunza Air Tag na AirPods Pro kwa pamoja

Kirusi kimepatikana!
Madhara ya virusi vya kompyuta si mageni kwa mtu amabaye anatumia kompyuta mara kwa mara. Virusi huharibu mafaili, huleta usumbufu, husimamisha kazi na huduma na inaleta hasara kibiashara. Pengine hujawahi kufikiria kwamba kirusi kinaweza pia kutumika bila kukudhuru moja kwa moja wala kukuletea usumbufu. Kuna virusi vinayoweza kutumika kukuibia taarifa zako binafsi ili kukutapeli, kughushi utambulisho wako na hata kukuletea fedheha.
Sababu kuu ya watu kupata virusi vya kompyuta ni kukosa elimu ya msingi au kutojali kulinda taarifa zilizopo kwenye kompyuta na vifaa-kompyuta. Watu wengi hupata virusi pale wanapohamisha vitu kutoka kwenye kompyuta inayotumika na jamii, yani zile kompyuta za steshionari, vibanda vya mtandao (‘internet cafe’) na zile za maofisini na mashuleni. Virusi huenezwa kwa njia ya mtandao. Utapata virusi kupitia kwa barua-pepe na  kurasa mbalimbali hatarishi kama kuarasa za picha na filamu za ngono na zile zitoazo programu za kushusha bure.
Wataalamu wanasema kuwa hakuna suluhisho la moja kwa moja la virusi vya kompyuta. Hii ni kwa sababu mbinu mpya za kushambulia kompyuta zinavumbuliwa na maprograma waharibifu kila siku. Hivyo basi, njia kuu ya kujilinda ni kuhakikisha una programu ya ‘anti-virus’ kwenye kompyuta au kifaa-kompyuta unachomiliki kama tahadhari. Antivirus ni programu amabyo hutumia mbinu mbalimbali kugundua virusi vya kompyuta ambavyo vinajulikana. Mifano bora ya antivirus ni pamoja na BitDefender, Kaspersky, Norton, AVG, na Avast. Pia, unashauriwa kuwa muangalifu pindi unapoingiza kifaa ulichotumia kwenye kompyuta nyingine kwenye kompyuta au kifaa kompyuta chako na pia kitu chochote unachoshusha kutoka kwenye mtandao. Hivi vyote unashauriwa kuvipekua kwa kutumia antivirus uliokuwa nayo.

Je, wewe unazingatia haya? Ni antivirus gani unajua kuitumia na unaiamini, kwa nini?


Antivrus

 

 

 

 

 

ecay

Ninafuatilia teknolojia kila siku na ninapenda kutoa ujuzi wangu kuhusu teknolojia. Karibu tuzungumze kuhusu teknolojia hapa teknokona!

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania