fbpx

Uvumi: Sony kuja na simu yenye display ya kukunjwa

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Kuna tetesi ya kwamba kampuni ya Sony ipo njiani kuja na simu yenye display ya kukunjwa. Tetesi hizo zinasema kwa sasa Sony wapo katika hatua za kutengeneza simu za mfano (prototypes) za kuweza kutambulishwa ifikapo Disemba mwaka huu.

Hii si mara ya kwanza kwa taarifa kama hizi kuja. Ila kwa sasa hivi taarifa zimekuja zikiwa na mambo mengi yanayohusiana na simu hiyo.

INAYOHUSIANA  Tegemea Kuback Up Chati Za WhatsApp Katika Google Drive!

Display/Kioo cha simu hiyo kinatengenezwa na kampuni ya LG – ambao tayari ni watengenezaji nguli pia katika teknolojia za display/vioo vya kielektroniki.

Teknolojia ya display itakayotumika itakuwa na uwezo wa kuvutwa na kuhifadhiwa katika hali mkunjo. Kwa kifupi Sony wanataka kutengeneza simu muundo wa kitofauti zaidi ukilinganisha na simu za display ya mkunjo kutoka Samsung – Fold, Huawei na Xiaomi.

INAYOHUSIANA  iOS10: kuja na mabadiliko kadhaa! #Apple #iOS

Baadhi ya sifa zilizovuja;

  • Kuna optical zoom 10x
  • Betri la mAh 3220
  • Prosesa ya Snapdragon 855
  • Uwezo wa 5G

Sony kuja na simu yenye display ya kukunjika

Watafiti wengi wanaamini simu hiyo haipo njiani kuja muda wowote wa karibu. Tuliona jinsi Samsung walivyorudi tena kiwandani kuboresha simu yao ya Samsung Galaxy Fold baada ya simu kadhaa kuharibika baada ya kutumika kwa muda mfupi tuu na waandishi wa habari.

INAYOHUSIANA  Fikiria Simu Bila Ya Betri, Teknolojia Hii Ipo Katika Hatua Zake Za Kwanza!

Je unadhani kuna umuhimu wa kuja na simu zenye display zinazoweza kukunjwa au unaona teknolojia ya sasa inatosha na zingebaki hivi hivi?

Vyanzo: Techradar na tovuti mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.