fbpx

Utafiti: Sababu inayosababisha ubongo kuamuru mtu kupiga miayo

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Ni jambo lililozoeleka kuwa mtu anapopiga miayo ni ishara ya kuwa anahisi uchovu au ana njaa na wakati mwingine vyote kwa pamoja lakini katika utafiti uliofanywa na wanasayansi hivi karibuni umegundua kitu ambacho hakikufahamika huko nyuma.

Swali la “Kwanini mtu hupiga miayo?” ambapo muuliza swali angetegemea kupata jibu la kisayansi zaidi limeweza kupata majibu na TeknoKona tunaamini baada ya kumaliza kusoma makala hii utakuwa umeelimika.

Timu ya watafiti katika Chuo kikuu cha Nottingham, imegundua sehemu ya primary motor cortex (ambayo ni sehemu ya ndani ya ubongo wa binadamu) pia inatumika sehemu kubwa wakati mtu anapopatwa na ugonjwa wa neva. Kupiga miayo mara kwa mara, ni dalili ya “Echophenomena – yaani namna ya kuiga maneno na matendo ya mtu mwingine bila kujua.

Transcranial magnetic simulation-mashine iliyotumika kuaini kitu gani hupelekea ubongo kuamuru mtu kupiga miayo.

Hali hii ya Echophenomena pia inaonekama kwa mtu anayeugua ugonjwa wa neva au mtu anayeugua kifafa na tawahudi. Katika uchunguzi wa wanasayansi watu 36 waliojitolea kufanyiwa uchunguzi  na walipokuwa wanafanyiwa uchunguzi wa kisayansi wengine walipiga miayo.

INAYOHUSIANA  Nepi janja zipo njiani kuingia sokoni; wenye watoto muwe tayari

Katika matokeo ya utafiti huo baadhi yao waliambiwa kuwa ni sawa mtu kupiga miayo, ilihali wengine wakiambiwa wajitahidi kuzuia hali hiyo kufanyika. Kwa ujumla, hamu ya kupiga miayo iliamuliwa kuwa ni namna kila motor cortex ya kila mtu inavyofanya kazi.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.