fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Kenya Sayansi

Kenya yafanikiwa kurusha saetelaiti yake ya kwanza

Kenya yafanikiwa kurusha saetelaiti yake ya kwanza

Spread the love

Nchi ya Kenya imeingia katika vitabu vya historia kwa kurusha Setilaiti yake ya kwanza angani kutokea nchini Japan.

Mapema wiki huu tulileta makala kuhusu Kenya kurusha satelaiti yao kwa mara ya kwaza. Raia wa Kenya walifuatilia tukio hilo moja kwa moja wakiwa mjini Nairobi siku ya Ijumaa.

SOMA PIA  NASA: Mwanamke ndio kuwa mtu wa kwanza kutua Mars (Mihiri)

Satallite hiyo imetengezwa na wanasayansi kutoka katika chuo kikuu cha Nairobi. chuo kikuu kimojawapo cha Italia wakiwa wameshirikiana na wanasayansi kutoka katika shirika la JAXA, Japan.

kurusha saetelaiti yake

Satelaiti ya kwanza kabisa kurushwa nchini Kenya.

Kufaulu kwa urushwaji wa satallite hiyo ni faraja kubwa kwa wanasayanzi wa Kenya. Satelaiti hiyo imegharimu kiwango cha fedha zaidi ya dola milioni moja. Nchi zingine za Afrika zilizowahi kurusha satelailaiti zake ni Misri, Afrika Kusini, Nigeria, Morocco na Algeria.

Satelaiti hiyo itatumika kwa kutoa taarifa tofuati kwa manufaa kwa Kenya kama kutoa tahadhari katika kukabiliana na majanga, kutoa taarifa ambazo zitasaidia katika kilimo.

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania