fbpx

Uchina kutengeneza vipuri vyake mwenywewe

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Vita ya kibiashara iliyoanzishwa na rais wa Marekani imesababisha Uchina kufikiria namna ya kupunguza kutegemea bidhaa za zinazotengenezwa kutoka kwenye taifa linaloongoza kiuchumi.

Uchina sasa imeamua kujifunga mkanda na kuamua kutengeneza vipuri ambavyo mizizi yake ni kutoka kwa AMD (processor) za 32 Bit ambazo zitafamika kama Dhyana.

AMD haiwatengenezei Uchina kisha kuwauzia bali imewaruhusu kutengeneza za vipuri hivyo vinavyotumika kwenye kompyuta kulingana na mahitaji ya nchi yao.

Dhyana-Kipuri kilichotengenezwa na Uchina kulingana na mahitaji yao ya kitu hicho kwenye kompyuta.

Mwaka 2015, Marekani ilizuia Intel pamoja na makampuni mengine yanayotengeneza vipuri vya kwenye kompyuta kwa sababu ya kuamini vitu hivyo vilikuwa vinachagiza Uchina katika utengenezaji wa silaha hatarishi sana (nuclear).

kutengeneza vipuri

Kipuri cha kompyuta kinachotengenzwa na AMD ambacho kinafanana kabisa na kile ambacho Uchina wanatengeneza tofauti yao ikiwa namba zinazozitambulisha.

Uamuzi wa AMD unaweza kufanya kazi na Uchina kunaleta maana kwamba sasa upinzani mkali upo mbioni kurudi ambao ulionekana kupotea kwa miaka kadhaa.

Vyanzo: Techspot, Hexus

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Simu za Huawei kukosa Google Playstore na huduma zingine za Google
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.