Imeelezwa kuwa WhatsApp sasa wana mpango wa kuongeza vipengele vipya zaidi viwili lengo ni kuzidi kuifanya programu tumishi hiyo kuwa bora zaidi kwa watumiaji wake.
Kipengele cha kwanza ni “Mark As Read” ambapo kitamuwezesha mtu kuweka kuruhusu meseji kuwa tayari amesoma bila kuifungua, ikitokea katika sehemu ya taarifa fupi (notification bar).
Kipengele cha pili ni “Mute” ambacho kitamuwesha mtu kuweza kuzima kupokea taarifa fupi bila kufungua WhatsApp; kwa ule ujumbe mfupi ambao unasomeka kikamilifu bila kufungua ndani hapa ndio mahala pake.
Kipengele cha kusema kuwa ujumbe umeshasomwa bila kufungua kimewekwa kwenye WhatsApp.
Baada ya kukosolewa vikali juu ya usambaaji wa taarifa za uongo kupitia WhatsApp, wameamua pia kuachia kipengele kipya ambacho kitatoa taarifa na kuonesha juu ya meseji ambazo imetumwa na mtu kama kaandika mwenyewe au kachukua kutoka sehemu nyingine (forwaded).
Sio kwa jumbe tu (messages) bali hata kwa picha na video, kipengele hicho kitafanya kazi ya kukuonesha uhalali na usahihi wa kitu kilichotumwa. Lakini pia, kwa upande wa usambazaji wa Links, itaweza kukujulisha kwa kukuwekea alama nyekundu kukuonesha kuwa makini na taarifa hiyo kabla hujaifungua.
Vipengele hivyo vipo kwenye WhatsApp Beta toleo la 2:18:214. Tuambie hapo chini katika sanduku la maoni, juu ya mabadiliko haya mapya? Unafikiri yatazidi kuvutia zaidi watumiaji wake?
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.