fbpx

Uber wawezesha utoaji wa bakshishi (tips) kwa madereva

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Kampuni ya huduma ya usafiri ya Uber imekuja na mfumo rasmi wa utoaji wa bakshishi yaani tips kwa madereva. Kwa sasa ilikuwa unaweza kumpa bakshishi ukijisikia ila kwa sasa itakuwa ni chaguo rasmi kwa wale wanaolipa kwa kadi kuunganisha moja kwa moja kwenye makato ya safari.

Huduma hii inakuwa ni nzuri kwa walipaji wa kadi ambao mara nyingi wanashindwa kumpa dereva bakshishi kama ikitokea wakiwa hawajabeba pesa taslimu. Pia itakuwa ni nzuri kwa madereva Uber wanaopokea wageni kutoka nje maeneo ya Airport ambao wanaweza wakawa hawajapata pesa za nchini na hivyo inakuwa rahisi wao kutoa tip/bakshishi kwa mfumo wa malipo ya VISA.

Uber wawezesha utoaji wa bakshishi

Uber wawezesha utoaji wa bakshishi : Mfumo wa kutoa tip kwa madereva wa Uber kwa mfumo wa malipo ya VISA

Ila si siri ya kwamba madereva wengi watapenda kupewa bakshishi ya pesa taslimu/keshi kuliko kupitia mfumo wa Uber, hili halijauziwa kwa ujio wa njia. Bado mteja ana uhuru kufanya hivyo.

INAYOHUSIANA  Mimi na Rais: Uzinduzi wa Kitabu unaoonesha Matumizi Bora ya Mitandao ya Kijamii

Msafiri kutumia kipengele hiki ni hiari kwa 100%, na utaweza kuona kiasi cha mapendekezo unachoweza kutoa ila bado unaweza kuweka kiasi utakacho wewe. Kipengele hiki kitakuwa sehemu ya chini ya tathmini na pongezi ya app. Malipo yote ya tip yatakatwa kwenye kadi ya benki ya msafiri iliyosajiliwa kwenye mfumo wa Uber.

Hivi ndivyo inavyofanya kazi:

  • Jinsi ya kumpa dereva tip
  • Pakua toleo jipya la app.
  • Mwishoni mwa safari yako, ongeza tip baada ya kutathmini safari yako.
  • Chagua mojawapo kati ya kiasi kilichowekwa au uweke kiasi unachotaka.
  • Bonyeza Nimemaliza ili utume tip yako.

Pesa zote za tip zitatumwa kwa dereva moja kwa moja, Uber haitatoza ada yoyote ya huduma kwenye tip.

Vipi wewe una mtazamo gani juu ya maboresho haya? Je ukitumia Uber huwa unapendelea kulipa kwa pesa taslimu au kwa malipo ya kutumia kadi za benki(VISA/Mastercard).

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.