Twitter inaleta uwezo wa ku ‘tag’ maeneo kwa kutumia App hiyo ya Twitter na kwa mtandao. Hili ni jambo jema kwa kuwa wakati mwingine mtu anahitaji kusema yuko wapi kwa kubofya tuu.
Kampuni ilituma tweet ambayo ilitambulisha ujio wa kipengele hiko na ushirikiano(Partnership) na Foursquare kwa kuonyesha video jinsi kipengele hicho kitakavyoweza tumika katika iOS.
Hapo awali huduma ya kutambulika ulipo kwa kutumia Twitter, Ilibidi twitter itumie ‘coordinate’ za mahali ulipo ili itambue hiyo sehemu. Hili lilifanikiwa kwa kuzingatia sensa ya kifaa chako na kuweza kupapatia jina (hapo mahali) kulingana na vitu vinavyokuzunguka
Twitter iliandika “Coming soon! We’re working with
@foursquare so you can tag specific locations in Tweets: ” kupitia ukurasa wake katika mtandao huo
Sasa watumiaji wa Twitter wataweza kubofya kutufe cha Mahali (Locations) moja kwa moja ili kuweza ku ‘Tag’ maeneo waliyopo. Ukibofya hicho kitufe zitatokea orodha nyingi za maeneo kisha utachagua eneo ulilopo.
Twitter ilisadikiwa kuwa na maongezi ya siri na Foursquare kuhusha jambo hili mwishoni mwa mwaka jana wakati Business Insider iliripoti kuwa huduma hiyo ya ku ‘tag’ maeno itaanza kutumika katika kipindi cha robo ya mwaka 2015.
Tweet ambazo zitakua na maeno zitawasaidia sana Twitter kama kampuni katika kukuza mfumo wake wa kuongeza kipato kwa kutumia matangazo (matangazo yatakua yanawafikiwa watu husika kirahisi). Twitter imeelezea zaidi huduma hii katika tovuti yake ya kutoa msaada, Bofya hapa kusoma
Wazo lako ni muhimu, ningependa kusikia kutoka kwako pia tafadhali ungana nasi kupitia kurasa zetu za Facebook ,Twitter, Na Instagram
No Comment! Be the first one.