fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Intaneti Kompyuta Maujanja Teknolojia

Tovuti za kupakua muvi mtandaoni

Tovuti za kupakua muvi mtandaoni
Spread the love

Kama unapenda kuangalia muvi basi endelea kusoma makala hii uweze kufahamu tovuti za kupakua muvi mtandaoni. Kuna tovuti nyingi za kupakulia muvi na tamthilia mtandaoni lakini hizi ndo maarufu zaidi.

YtsHii ni tovuti maalum kwaajili ya kupakulia muvi zenye ubora wa hali ya juu (HD). Unapoingia katika tovuti hii utakutana na orodha ya muvi mpya zilizotoka lakini pia utaweza kutafuta muvi za zamani katika sehemu ya kutafuta na kuipakua. Pia unaweza kuangalia trela ya muvi kabla haujaipakua na kusoma maelezo mafupi kuhusu maudhui ya muvi hiyo pamoja na waigizaji waliopo katika muvi hiyo.

Tovuti za kupakua muvi mtandaoni

Muonekano wa tovuti ya yts

PiratebayTovuti hii ni maarufu sana, unaweza kupakua mambo mbalimbali ndani ya tovuti hii kama muvi, tamthilia, gemu, programu za kwenye kompyuta, vitabu na mambo mengine mengi. Hautaweza kuona picha wala kupata maelezo yoyote ya ziada kuhusu kitu unachokipakua unapokuwa kwenye tovuti hii. Unashauriwa kuchukua tahadhari dhidi ya wadukuzi unapotembelea na kupakua mafaili katika tovuti hii.

SOMA PIA  Punguzo la bei ya betri kwa simu za iPhone

13337xTovuti hii pia huwa na mambo mengi kama muvi, tamthilia pamoja na programu za kompyuta. Unapotaka kupakua muvi katika tovuti hii unatakiwa kuitafuta kwanza katika sehemu ya kutafutia halafu ukiiona utaibonyeza na kupelekwa katika kurasa ya kupakulia hiyo muvi. Hautaweza kuona picha yoyote wala maelezo ya ziada kuhusu hiyo muvi unayotaka kupakua.

SOMA PIA  Kingo Root: Programu/App ya Kuroot Simu za Android na Windows

KissasiansTovuti hii ni maalum kwaajili ya muvi na tamthilia za kikorea na kichina. Unapotembelea tovuti hii utaweza kuona muvi na tamthilia mpya za kichina na kikorea lakini pia unaweza kutafuta muvi hizo kupitia sehemu ya kutafutia. Tovuti hii inaruhusu kuangalia moja kwa moja mtandaoni  na pia kuipakua hiyo muvi au tamthilia unayoitaka.

SOMA PIA  Nubia Alpha: Simu janja inayovaliwa mkononi

O2tvseriesHii ni tovuti maalum kwaajili ya kupakua tamthilia mbalimbali nyingi zikiwa ni za marekani. Unapotembelea tovuti hii utaona orodha ya tamthilia zote zilizopo kwenye tovuti hiyo na utaweza kujichagulia ni tamthilia ipi ungependa kuipakua. Sifa kubwa ya tovuti hii ni kwamba unaweza kupakua na kuangalia tamthilia kupitia simu janja yako.

Tovuti za kupakua muvi mtandaoni

Muonekano wa tovuti ya O2tvseries

Endelea kutembelea tovuti yetu uweze kujifunza mambo mbalimbali kuhusu teknolojia na pia kupata uelewa zaidi wa matumizi sahihi ya huduma za mtandaoni. Soma makala zetu nyingine hapa.

Semu Msongole

Digital Marketing Strategist, Content Writer, and Social Media Manager at Teknokona Blog.

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania