Imekuwa kama desturi kwa Microsoft kutoa toleo jipya la programu endeshi-Windows kila baada ya mwaka lakini hilo litakalofuata inaaminika kuwa litatoka miaka miwili kutoka sasa (2024).
Taarifa zinasema kwamba Microsoft wana mkakati wa kufanya mabadiliko katika utaratibu wao wa kutoa maboresho ya mfumo na matoleo mapya. Hili lilionekana ambapo kutoka toleo la Windows 8 mpaka Windows 10 ilipita zaidi ya miaka miwili. Kutoka Windows 10 hadi Windows 11 ilipita miaka sita (2015 mpaka 2021). Kati ya miaka hiyo kulikuwa na maboresho kadha wa kadha ili kuiimarisha mifumo hiyo.
Microsoft sasa inatarajiwa kubadilisha hali hiyo ambapo inatazamwa kutoa maboresho ya mfumo kila baada ya miezi mitatu ikimaanisha mara nne kwa mwaka. Pia kutoa toleo jipya la programu endeshi kila baada ya miaka mitatu. Kwa kuzingatia Windows 11 ilitolewa Oktoba 2021, matarajio ni kuwa toleo linalokuja na inaaminika kuwa litaitwa Windows 12 kutoka kwenye nusu ya pili ya mwaka 2024.

Microsoft ina mpango wa kuendelea kuifanya Windows 11 kuwa madhubuti kwa kutoa masasisho ya mara kwa mara ambapo kati ya mwezi Septemba au Oktoba yatatolewa maboresho makubwa. Halikadhalika, mwaka 2023 Windows 11 itaendelea kufanyiwa maboresho katika kipindi cha mwaka mzima.
Haya sasa kama wewe bado unatumia Windows 7, 8, 8.1 sijui kompyuta yako ina hali gani huko maana haipokei masasissho kutoka Microsoft kwa sababu matoleo hayo yameshatolewa kwenye mpango wa kuziboresha.
Vyanzo: The Verge, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.