fbpx
apps, Gemu, Microsoft

Netflix ya Magemu? Microsoft waja na huduma ya malipo ya mwezi, magemu 100+

netflix-ya-magemu-microsoft-game-pass
Sambaza

Netflix ya magemu? Microsoft watambulisha huduma ya magemu kwa malipo ya mwezi inayoonekana kwenye njia ya kupata mafanikio. Hii unaweza kusema ni Netflix ya magemu, kwa kuingalisha na huduma ya malipo kwa mwezi kwa ajili ya muvi/filamu ya Netflix.

Huduma ya Netflix ni nini? Fahamu huduma hii ya kuangalia muvi mtandaoni

netflix ya magemu xbox game pass

Huduma ya Microsoft kwa ajili ya magemu inaenda kwa jina la Xbox Game Pass.

Huduma ya Xbox Game Pass inapatikana kwa watumiaji wa mashine ya magemu ya Xbox na pia inapatikana kwa watumiaji wa kompyuta za Windows. Kwa wanaomiliki vifaa vyote viwili watalipa bei kubwa tofauti na wale wanaotaka kutumia kwenye kompyuta tuu.

INAYOHUSIANA  Unamfuatilia kisiri mtu Instagram? Instagram wafanya iwe vigumu!

Kupitia huduma hii ya XBox wanalenga kufanya iwe rahisi zaidi kwa watu wanaopenda magemu ya kompyuta kuweza kupata magemu kwa bei nafuu zaidi – kwani badala ya kutumia pesa nyingi kununua gemu moja moja sasa wataweza kulipia malipo ya mwezi na kupata magemu zaidi ya 100 kwenye vifaa vyao.

xbox game pass magemu
Baadhi ya magemu yanayopatikana, yapo magemu mengi sana hii ikiwa ni pamoja na Mortal Kombat mpya na mingine mengi maarufu – orodha nzima inapatikana kwenye tovuti ya Microsoft/XBOX Game Pass

Malipo kwa sasa yanaanza kwa takribani Tsh 23,000 kwa mwezi ($9.99). Kwa sasa huduma imeanza na magemu kutoka watengenezaji magemu zaidi ya 75 (watu binafsi na makampuni).

INAYOHUSIANA  Rais wa Urusi Vladimin Putin hatumii kabisa simu janja

Je una mtazamo gani katika huduma ya kupata mamia ya magemu bure kwa malipo ya kila mwezi? Huduma hii inapatikana moja kwa moja kupitia tovuti yao ya Microsoft – XBOX Game Pass

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |