fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Android apps Maujanja simu Teknolojia

Washa tochi/kamera ya kwenye simu janja kwa kuitikisa tuu

Washa tochi/kamera ya kwenye simu janja kwa kuitikisa tuu

Spread the love

Simu janja zimekuwa msaada kwetu kwa mambo mengi ambayo zimekuwa zikirahisisha shughuli kadha wa kadha kwenye ulimwengu huu wa teknolojia. Ile taa ya kuongeza mwangaza pembeni ya kamera ya nyuma ni tochi pia ambayo unaweza kuiwasha kiurahisi kabisa.

Uwepo wa taa pembeni ya kamera imekuwa na kazi zaidi ya moja na wale ambao tunapenda kuongeza ubora wa picha kabla ya kupiga ama inatokea upo sehemu yenye mwanga hafifu na unahitaji msaada wa kuona kitu fulani vizuri hakika tunashukuru kwa simu janja zetu kuwa na kitu ambacho kimewekwa kwa ajili ya kazi hiyo.

SOMA PIA  Fahamu kuhusu Spyware

Sasa inatokea wakati fulani unatamani upate wepesi wa kuwasha/kuzima tochi au kamera bila ya kufuata hatua ambazo sote tunazifahamu lakini inakuwa haiwezekani. Changamoto inapotokea ndio inakuwa chachu ya kutafuta jibu la kitu fulani na kutokana na ukuaji wa teknolojia suala zima la kuwasha ama kuzima iwe tochi au kamera ni rahisi kabisa.

Fahamu kuhusu Shake Flashlight & Camera

Shake Flashlight & Camera ni programu tumishi inayopatikana kwenye Playstore ikiwa imetengenzwa kumwezesha mwenye simu janja ya Android kuwasha/kuzima tochi au kamera kwa kuitikisha tu kwa mara kadhaa. FUata hatua hizi ili uwe unaweza kuwasha na kuzima kamera/tochi kwa urahisi sana:

SOMA PIA  Tovuti za kupakua muvi mtandaoni

>Mara baada ya kupakua programu tumishi husika (Shake Flashlight & Camera) ifungue na utauona ujumbe utaojitokeza kuhusu matumizi ya betri kwenye programu tumishi hiyo. Unaweza kuchajua Cancel kwa maana ya kuupuzia kile kilichoelezwa au ukachagua “Don’t show again” na kubofya “Disable“.

tochi

Kitu cha kwanza kinachoonekana baada ya kufungua programu tumishi-Shake Flashlight & Camera ambapo unaweza kuchagua kubofya Cancel au Disable.

Hatua ya pili ni kuwasha kitufe (kupeleka upande wa kulia) kwa maana ya kuruhusu (on) kwenye kipengele cha tochi (Flashlight). Halikadhalika, utafanya hivyo hivyo iwapo utapenda pia kuwasha kamera kwa kuitikisha tu.

tochi

Jinsi ya kuwasha au kuzima kamera/tochi kwa kutikisha tu.

Ikitokea unapenda kuzima kipengele hicho kisifanya kazi tena au hutaki kuwa na programu tumishi kwenye simu yako basi unazima vipengele husika (weka off) kisha iondoe programu tumishi kama ambavyo huwa unaondoa nyingine.

Pakua Shake Flashlight & Camera

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania