fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Android Google

Android N: Toleo jipya la Android kuja na mambo mapya

Android N: Toleo jipya la Android kuja na mambo mapya

Spread the love

Google wametoa toleo la majaribio la Android toleo la saba maarufu kama Android N ambalo litasambazwa kwa watumiaji wote katika robo ya tatu ya mwaka huu. Toleo hili linatoa mwanga fulani juu ya toleo lijalo la Android ambalo bado halijapatiwa jina.

Ingawa toleo lililo tangulia la Android Marshmallow linatumiwa kwa asilimia 2.3 tu kwa sasa, Google tayari wamejikita katika ujio wa toleo jingine la Android litakalokuja baada ya Marshmallow. Kwa sasa linafahamika kama Android N na tayari unaweza fahamu machache yanayotegemewa kuja katika toleo hilo.

SOMA PIA  Youtube Wazindua Huduma Ya 'Live Stream' Kwenye App Ya Simu Kwa Majina Makubwa!

Toleo Jipya la android

Badilko kubwa ambalo limeripotiwa na mitandao ambayo imekwisha jaribu toleo jipya la Android ni lile la kuwa na uwezo wa kuendesha app zaidi ya moja katika screen moja, hii sasa itawawezesha watumiaji wa Adroid kuweza kuendesha app zaidi ya moja kwa wakati mmoja.

Hii itakuwa ni zaidi ya uwezo tulio nao wa kutumia app moja wakati nyingine inaendelea kufanya kazi kwani kwa sasa utaweza kuziona app zote mbili zikiwa zimegawana screen nusu kwa nusu. Huu ni mtindo ambao Windows wamekuwa wakiutumia kwa muda mrefu sasa.

SOMA PIA  Bill Gates asema anatumia simu ya Android, Ni samsung Galaxy S8?

Pia toleo hili litakuja na mfumo mpya wa uchezwaji wa video na moja ya vitu vipya ni uwezo wa kucheza video huku mtumiaji akiweza kufanya mambo mengine kama vile kuchagua video nyingine ya kuchezwa. Uwezo huu unafanana na ule ambao unapatikana katika app ya Youtube, toleo hili litaruhusu utaratibu huo ambao umekwisha tumiwa na Youtube pamoja na iOS.

Kama hayo hayatoshi Android N itakuja na uwezo wa mtumiaji kujibu Notification yeyote moja kwa moja kutoka katika Notification bar yaani hakutakuwa na haja ya kwenda kufngua ujumbe ili uujibu bali pale pale katika notification unaweza kujibu ama kuipotezea. Huu utaratibu watumiaji wa iOS wamekuwa nao kwa muda mrefu sasa ila kwa watumiaji wa Android hii ndiyo itakuwa mara yao ya kwanzaa.

SOMA PIA  App Bora Kwa Ajili Ya Kamera Za iOs Na Android!

Yapo mambo mengine madogo madogo ambayo pia yameboreshwa katika toleo hili jipya lililokwenye matengenezo, endelea kutembelea TeknoKona na tutazidi kukupa habari zaidi kulingana na maendeleo ya toleo hili la Android.

Tungependa kusikia kutoka kwako kati ya hayo yote ambayo Google wanayalenga kuyaingiza katika Android toleo jipya lipi ambalo limekuvutia zaidi

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania