Ni wazi kuwa Android imejibadilisha kwa kiasi kikubwa na hii ukizingatia toleo jipya lina maboresho mengi tuu.
Hata iOS nayo imeongeza vipengele kibao na hivyo watu wanasema imeanza kuonekana kama Android tuu…wewe una nene lolote juu ya hilo?
Lakini unaweza ukawa unajiuliza hilo litafanikiwa vipi? Matangazo katika ‘lock screen’? ….

Kuna kampuni inayoyojihusisha na matangazo ya kidijiti ijulikanayo kama Glance, kwa sasa kampuni hii ina mpango wa kunzisha huduma ya matangazo katika uwanja wa ‘lock screen’.
Kwa kaunzia wanadai kuwa wataanzia marekani pengine mwezi wa nane, Glance inasemekana kuwa katika maongezi na makampuni mengi yanayotoa huduma ya mawasiliano.
Kingine cha kufahamu hapa ni kwamba Glance sio App yaani huwezi ukaingia katika soko la playstore na kuishusha baili itakua inaelea juu juu ya Android.

Lakini sio lazima uweze kuaingia katika kila unachokiona (matangazo) tuu katika ‘Lock screen’ yaani hapa unaweza ukatoa loki ukaendelea na mambo yako kama kawaida.
Kingine ni kwamba ukiwa katika ‘lock sreen’ hiyo yenye matangazo na mambo mambo mengine bado unaweza kushuka na kupanda juu ili kuangalia angalia vitu vingine.
Nna Imani sio mara kwa kwanza kupata matangazo juu ya ‘lock screen’ sio na mengine yanakuaga katika mfumo wa ‘Notification’
Ningependa kusikia kutoka kwako, je wewe unaweza kuwa tayari kutumia Android yenye mfumo huu? Niandikie hapo chini katika eneo la comment
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.