fbpx
simu, Tecno

TECNO Yaimarisha Ushirikiano Wake Na Google Kupitia #Camon12Pro! #CES2020

tecno-na-google-katika-ces2020

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

TECNO imeshiriki katika maonyesho ya teknolojia yanayojulikana kama Consumer Electronics Show (CES) kwa mwaka 2020. Katika maonyesho hayo kampuni hiyo ilikua na mengi ya kusema pamoja na hili la kuimarisha ushirikiano wake na kampuni ya Google.

Toleo jipya la simu CAMON 12 Pro Kutoka TECNO hivi karibuni limewekewa  kitufe cha ‘Msaidizi wa Google’ (Google assistant) ambacho kinaruhusu watumiaji kufanya mambo mengi zaidi kwenye mfumo wa Google.

Kampuni kinara ya Kimataifa ya simu za rununu ya TECNO yenye simujanja yake  ya  Camon 12 Pro ya hivi karibuni, inayowezeshwa na mfumo wa uendeshaji wa Pie ya Google (Android 9), imeweka kitufe cha Msaidizi wa Google (Google assistant) kwenye CAMON 12 Pro katika mkutano wa maonesho ya teknolojia ya mwaka 2020  (CES2020) Januari hii.

Google ikionesha Simujanja zenye kitufe cha Google Assistant kwenye banda lake katika mkutano wa maonesho ya teknolojia 2020.
Google ikionesha Simujanja zenye kitufe cha Google Assistant kwenye banda lake katika mkutano wa maonesho ya teknolojia 2020.

TECNO imejiunga na kuwa mshirika  wa Google kuleta mfumo mpya wa uendeshaji kwa wateja wake. Wakati Google inafanya maboresho ya mfumo endeshi (Android) kwaajili ya kuleta ufanisi madhubuti kwenye vifaa janja vipya vya kisasa, TECNO ilizindua simu mpya ya kisasa ya CAMON 12 Pro kwa kuweka Kitufe cha Google assistant  ambayo ilioneshwa kwenye kibanda cha Google katika mkutano wa maonesho ya teknolojia 2020 ili kusaidia watumiaji kufanya mambo kwa haraka zaidi na kupangilia vitu muhimu kwenye ratiba ambavyo vinavyoweza kufanyika baadaye.

“TECNO inawasisitiza watumiaji wake kujihusisha kikamilifu na matumizi ya vifaa vyake na programu za ndani,” alisema Stephen HA, rais wa TRANSSION na Mkurugenzi Mtendaji wa TECNO “Tunafurahi kuanza ushirikiano huu na Google.”

Simu hii mpya  ina kamera tatu nyuma ambazo zina 16 + 2 + 8MP AI Max Triple, pia ina mapinduzi ya kuonyesha-alama ya kidole kwenye skrini na mfumo wake wa uendeshaji yaani Android™ Unasaidia kufanya yafuatayo:

INAYOHUSIANA  Simu Mpya Za Firefox Kuja Afrika

Multi-camera support na camera updates: Kwa kamera zake tatu za nyuma, mtumiaji hufurahia picha iliyokuzwa isiyo na ukungu, atafurahia pia bokeh na mwonekano sawia wa picha.

AR Emoji: Watumiaji wa CAMON 12 Pro wanaweza kuboresha emoji zao wanazopenda na mwonekano halisi wa uso.

Matumizi ya Meseji Yaliyoboreshwa: Watumiaji wanaweza kujibu ujumbe au kuingiza maandishi mengine mapya moja kwa moja kutoka kwenye arifa (notifiction). Mfumo endeshi ambao ni Android ™ 9 Pie ndani ya CAMON 12 Pro sasa una uwezo wa kuonesha picha kwenye Arifa za Kutuma ujumbe katika simu.

INAYOHUSIANA  Kampuni Ya Simu Janja, Vivo Kudhamini Kombe La Dunia!

Mpangilio wa mkondo arifu uliorahisishwa: Watumiaji wanaweza sasa kuzuia makundi (groups) yote katika mipangilio ya arifu kwenye app. Android ™ 9 Pie sasa inatuma taarifa au hutoa kiashiria wakati hali ya kuzuia makundi kwenye arifu inapobadilika.

Kitufe cha Google Assistant: Ukiwa na Google Assistant, watumiaji wanaweza kudhibiti kazi, kuwasiliana, kupata majibu ya wanachouliza na kudhibiti mienendo ya nyumbani popote uendapo. Pia husaidia watumiaji kupangilia mambo yao ya kufanya baadaye, kuhifadhi kazi za kufanya baadaye na kukumbushwa na Google Assistant wakati wa kuzifanya unapokuwa umefika moja kwa moja kwenye skrini ya simu. Ili kuanza, sema tu “Halo Google” au bofya Kitufe cha Google Assistant.

TECNO CAMON 12 PRO yenye Kitufe cha Google Assistant
TECNO CAMON 12 PRO yenye Kitufe cha Google Assistant kama ilivyooneshwa kwenye kibanda cha Google.

TECNO imeonesha uwezo wake mkubwa kwa kuongoza na kwenda sambamba na mahitaji ya watumiaji wake katika kutimiza kiu ya teknolojia mpya kabisa inayotamba kwa sasa kulingana na tafiti na Maendeleo. TECNO itaongeza zaidi ushirikiano wake na Google ili kuwapa wateja huduma nzuri zaidi na simu za kisasa zenye teknolojia ya juu kabisa.

INAYOHUSIANA  Google kuacha kutoa masasisho kwenye simu janja mbili!

Kuhusu Kampuni ya Simu ya TECNO

Kampuni ya Simu ya TECNO ni kampuni tanzu kinara na bora kutoka TRANSSION Holdings. Ikienda kwa kaulimbiu yake ya “Expect More” yaani Tarajia Zaidi, Kampuni imejizatiti kikamilifu kuwapa watu simu za kisasa zenye teknolojia ya juu kwa bei wanayoweza kuimudu pia imedhamiria kuruhusu watumiaji kuvuka mipaka yao ya sasa na kugundua ulimwengu mpya wenye fursa zinazowezekana. TECNO inaelewa mahitaji ya watumiaji kutoka katika masoko tofauti na inawapa uvumbuzi wa vifaa mbalimbali vya mawasiliano zikiwemo simujanja, tablets na simuvitochi. TECNO ni Kampuni Kubwa ya Kimataifa na ipo katika masoko yanayoinukia zaidi ya  60 kote ulimwenguni. Pia ni Mshirika rasmi wa Kimataifa wa Klabu ya Mpira miguu ya  Manchester City.

Je, una maoni gani kuhusu teknolojia hii? Niandikie hapo chini sehemu ya comment, Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Hashdough

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com