Kama umejaribu kununua umeme katika hizi siku mbili kupitia kwenye baadhi ya wakala au kwenye makampuni ya simu kama Mpesa, Tigo Pesa na ata Airtel Money utakuwa umegundua jambo hilo haliwezekani kwa sasa. Sababu kuu ni kwamba shirika la Tanesco limevunja mkataba na mmoja wa mtoa huduma hiyo ya ununuzi wa Luku, kampuni ya Selcom.
Hali ilivyokuwa:
- Manunuzi yote ya luku yalikuwa yakifanyika kupitia mitambo ya makampuni mawili, Maxcom na Selcom.
- Makampuni haya ndiyo yanayowapa wengine kama vile mitandao ya simu na mabenki uwezo wa kununua na kulipia huduma ya umeme -Luku
- Hivyo mara nyingi pale ulipokuwa unapata shida kununua umeme inakuwa pale ambapo mfumo wa malipo unaotegemea mitambo ya moja ya hizi kampuni mbili unakuwa na hitilafu.
Tanesco kupitia amri ya WAZIRI wa Nishati na Madini, George Simbachawene, na ushauri wa TRA wamevunja mkataba wa uwakala na Kampuni ya Selcom. Sababu kubwa zilizotolewa ni kutokana na mitambo yake ya kuuza LUKU kuwa na matatizo ikiwemo matatizo ya kisheria katika kulipa kodi.
Inasemekano kero nyingi za ukosekaji wa huduma ya manunuzi ya LUKU ambayo imekuwa ikitokea hivi karibuni imekuwa ni kutokana na mitambo ya kampuni hii kusumbua.
Je utaweza kununua simu kupitia huduma za simu tena?
Kwa kuwa kabla ya hili kutokea makampuni ya simu na baadhi ya mabenki yalikuwa yanatoa huduma hiyo ya ununuaji wa umeme wa LUKU kupitia mitambo ya Selcom kwa sasa utaendelea kukosa huduma hiyo. Ila kama kutakuwa na uwezekano wa haraka makampuni haya kupata huduma hiyo kupitia mitambo ya Maxcom basi utaweza kupata huduma hiyo mara moja.
No Comment! Be the first one.