fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Mtandao Mtandao wa Kijamii Soundcloud

Soundcloud Yapunguza Asilimia 20 Ya Wafanya Kazi!

Soundcloud Yapunguza Asilimia 20 Ya Wafanya Kazi!

Spread the love

Pengine mwaka huu tunaweza tukawa ndio tumetangaza makampuni mengi kusitisha kazi wafanya kazi wake kuliko miaka mingine, haya sasa hii ni zamu ya Soundcloud.

Kwa upande wa Soundcloud unasema kuwa swala hili ni swala ambalo kampuni imeamua ili kutetea mapato katika kampuni maana tumeona makampuni mengi ya teknolojia yakiwa yanapata mapato kidogo kuliko matarajio yao.

Soundcloud

Soundcloud

Pengine hii inaweza kuwa sio sababu tosha, pengine kuna nyingine nyingine nyingi tu lakini bado kampuni imekazia kuwa ni sababu ya kampuni kushuka kiuchumi.

Kama unakumbuka mwaka 2017 tuu kampuni ilipunguza wafanyakazi kwa asilimia 40 na sasa wanakuja kwa asilimia 20.

SoundCloud

SoundCloud

Hii pengine inaweza ikawa ni kwa sababu kwa sasa mitandao ya huduma za ku”stream muziki na shughuli zingine za kistarehe ziko nyingi sana na hivyo zinaleta ushindano mkali sana.

SOMA PIA  Matangazo, Mpaka Ndani Ya Maduka Katika Mtandao Wa Intstagram!

Kuna kipindi kama sikuosei Sound Cloud ilikua ni moja kati ya mitandao maarufu kabisa katika swala zima la miziki katika mtandao.

Muonekano Wa SoundCloud Kwa Ndani

Muonekano Wa SoundCloud Kwa Ndani

Kwa kipindi cha nusu ya mwaka ya kwanza ni makampuni mengi ya kiteknolojia yamepata mapato machache ukilinganisha na walichotegemea.

SOMA PIA  Zoom Yainunua Kampuni Inayofanya Tafsiri Za Papo Kwa Papo!

Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la comment, je unadhani kwa mtandao wa Soundcloud kupunguza asilimia 20 ya ajira ni suluhisho?

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii

Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn

Hash

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania