Sony imaweka wazi kuwa imezindua simu janja ijulikanayo kama Xperia Z5 Premium ambayo inakuja katika rangi ya waridi (pinki). Simu hii ina sifa kede kede na TeknoKona tumekuandalia baadhi ya sifa hizo.
Sony wamewaweka wazi watu juu ya uzinduzi huo kupitia akaunti yao katika mtandao wa kijamii wa Twitter. Katika tweet hiyo kampuni pia liliambatanisha picha ambayo inaonyesha simu hiyo.
Celebrate style that’s strictly on your terms… Introducing #Xperia Z5 Premium Pink. https://t.co/qz1AQMOd55 pic.twitter.com/6WbIPdEdHN
— Sony | Xperia (@sonyxperia) April 12, 2016
Simu hii itakuwa na programu endeshaji ya Android 5.1 na pia itakuwa na uwezo wa kujikinga na maji (water proof). Pia itakuwa na uwezo wa kukaa na betri hadi siku mbili
Taarifa iliyopo ni kwamba ubora wa kioo chake ni ule wa 4K. Mwanzoni kabisa kampuni lilitangaza januari kupitia akaunti yake ya instagramu kuwa litakuja na simu ya pinki katika mfululizo wa simu zake za Xperia.
Kampuni inasema kuwa simu hizi zitaanza kupatikana katika masoko ambayo yamepangwa kuanzia mwezi mei. Bei na siku kamili ya kuanza kuuza simu hii haikuwekwa wazi na kampuni la Sony. Lakini tunaweza tukasubiri kumbuka mei ni kesho tuu!
Simu hii inatoka kama toleo la mbele ya Sony Xperia Z5 hivyo tegemea maboresho zaidi katika toleo hili. Rangi ya pinki ilikuja baada ya mbunifu wa kampuni la sony, Murai-san kuona kwamba watumiaji wa sony za mfumo wa ‘Premium’ inawabidi wapate rangi ya pinki katika vifaa vyao.
Soma uchambuzi wa kina wa Sony Xperia Z5 Premium – Kamera ya Megapixel 23, Kioo cha 4K: Ifahamu SONY XPERIA Z5 PREMIUM
Mpaka sasa bado hakuna maelezo juu ya mambo mengi kuhusiana na simu hiyo kama vile taarifa nyingi za uchambuzi kwani bado haijafika sokoni. Mpaka ikifika kaa mkao wa kula ili kupokea uchambuzi huo kutoka katika mtandao wako pendwa wa TeknoKona