Taarifa za hivi karibuni ni kwamba kampuni ya Playstation imenunua kampuni ya Bungie ambayo inamiliki gemu la Destiny.
Kampuni ya Sony ambayo ndio inamiliki Playstation imeweka wazi kuwa inataka kutumia asilimia 49 ya bajeti ya maendeleo ya Playstation katika kuhakikisha kuwa wananunua makampuni mengi zaidi.
Hii inamaanisha kuwa mpaka kufikia mwaka 2025 Sony kupitia Playstation itakua na magamu kibao. Magemu ambayo kwa sasa wanalengo kubwa la kuwa na magemu yale ya mfumo wa ‘live’.
Kwa sasa hakuna taarifa za juu ya magemu ambayo yatapata mfumo huu wa “live’ lakini fununu nyingi zinaonyesha kuwa yatakua ni yale ya God of War, Horizon Forbidden West, Spider-Man, The Last of Us na Uncharted.
Kumbuka magemu hayo hapo juu ni makubwa na yameleta pesa nyingi sana katika kampuni ya Sony na baadhi yake yana mpaka matoleo ya filamu, vitabu, katuni, midoli na machapisho mengine.
Bungie inasifika sana baada ya kutoa game lake maarufu sana la Halo (ambalo kwa sasa lina mpka filamu na mchezo wa kuigiza unaojulikana kwa jina hili).
Kikubwa ambacho kampuni inataka ni kuwa na magemu mengi amabayo wachezaji wanaweza kucheza ‘live’ na wakiwa wengi (multiplayer) mfano mzuri ni michezo kama Call Of Duty na WarCraft.

Kwa makampuni mengi yanayojihusisha na soko hili, jambo la kucheza michezo hii ‘Live’ ni jambo kubwa sana na mara nyingi huwa ni moja kati ya sehemu kubwa ambayo inaingizia kampuni kipato maana kuna ulipiaji wa huduma hii.
Ningependa kusikia kutoka kwako, nindikie hapo chini katika eneo la comment, je unahisi kampuni itanunua kampuni gani nyingine ili kufikia dhima yake?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.