fbpx

Snapchat kuleta selfie za 3D baada ya kununua Seene

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Ni wazi kwamba mtandao wa kijamii wa Snapchat unashika kasi sana kwa sasa miongoni mwa mitandao ya kijamii. Na sasa Snapchat wapo mbioni kuleta kitu kingine ambacho bado hakijawahi kufanywa na mitandao mikubwa.

seene

Muonekano wa app ya seene

Snapchat wamenunua app ya kupiga picha za 3D kirahisi ambayo naitwa Seene.  App hii inawawaezesha watumiaji wake kupiga picha za 3D kwa kutumia kamera ya simu bila ya kuhitaji sensor za aina yeyote ile.

INAYOHUSIANA  Usalama mkubwa kwenye app ya Telegram: Sasa una uwezo wa kufuta chati nzima

Mitandao kama Google na Microsoft imekuwa ikifanya majaribio ya huduma ambayo inafanana na huduma ya app hii lakini vyote Project Tango ya Google na Kinect ya Microsoft zina hitaji sensor ili kupiga picha za 3D. Ingawa bado teknolojia ambayo inatumiwa na Seene haijawa wazi lakini ni dhahiri kwamba app hii inafanya kile ambacho Google na Microsoft wanafanya lakini kwa gharama nafuu na urahisi mkubwa.

INAYOHUSIANA  Jinsi ya Kuikatalia WhatsApp kutuma data zako kwenda Facebook

seene

Kama Snapchat wataingiza teknolojia za app hii katika app yao ya basi watumiaji wake wataweza piga picha za 3D na kuzishare kitu ambacho kitaongeza utamu zaidi katika mtandao wa kijamii huu unaokua kwa kasi kwa sasa.

Soma – Snapchat sasa ina wastani wa watumiaji wengi kwa siku kuzidi Twitter

Msomaji jiandae kusnapchatika na picha za 3D napia usisahau kutu add katika snapchat yako ili tunatumia jina la @Teknokona.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

Comments are closed.