fbpx
apps, Snapchat

Snapchat Imekua ‘Chombo Cha Uhariri’ Zaidi, Kuliko Mtandao Wa Kijamii!

snapchat-imekua-chombo-cha-uhariri-zaidi-kuliko-mtandao-wa-kijamii
Sambaza

Ni wazi kuwa Snapchat ilikuja kwa kishindo kikubwa sana, wengi walikua na matagemeo makubwa sana kuhusiana na mtandao huu. Sio kwamba mtandao haufanyi vizuri, lakini haufanya vizuri sana kama ilivyokuwa matarajio ya wengi.

Kwa sasa wengi wana Snapchat katika simu zao au wana Account za Snapchat lakini hawatumii mara kwa mara mtandao huo, au pengine hawatumii kabisa.

Pengine unaweza ukadhani watu wameamua kuanza kupotezea  mtandao huo baada watu maarufu kama Rihanna kukwazana na Snapachat au baada ya mwanamitindo maarufu Kylie Jenner kusema kwamba kwa maoni yake anaona mtandao huo umekufa.

INAYOHUSIANA  PowerAmp 3.0 : App bora ya kusikilizia mziki yazidi kung'aa
Na Snapchat Ulianza Baada Ya Mtandao Ku'post Hivi
Mgogoro Wa Rihanna Na Snapchat Ulianza Baada Ya Mtandao Ku’post Hivi.

Mtazamo wangu naona kama mtandao huu sana sana unatumika kama uwanja wa kuhariri (ku’edit) picha na video na kisha watumiaji huwa wanachapisha picha/video hizo katika mitandao mingini ya kijamii kama vile WhatsApp, Instagram na Facebook.

Kumbuka inawezekana Snapchat kuwa mtandao namba moja ambao ulikua na ‘Filter’ nyingi na nzuri kuliko mingine ndio maana Facebook na Instagram waliiga hii kitu. Licha ya hivyo picha na video ambazo zina ‘Filter’ za Snapchat bado zinaonekana katika mitandao mingine

INAYOHUSIANA  Mawasiliano ya Skype yanayohusisha watu wengi zaidi

Kumbuka kuna watu pia huwa wanatumia tuu kamera ya Snapchat katika kujipiga picha wakidai kamera ya mtandao huu ni nzuri.

Niambie wewe unalionaje hili je, lina usahihi? Ningependa kusika kutoka kwako. Niandikie hapo chini sehemu ya maoni.

Usisahau kutembelea TeknoKona kila siku ili kujipatika habari kede kede zinazohusiana na teknolojia na sayansi kwa ujumla. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: ,

Hashdough

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com