fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

tecno

Huawei simu Uchambuzi

Uchambuzi wa simu ya Huawei Y5 Prime 2018. Uwezo na Sifa

tecno

Simu ya Huawei Y5 Prime toleo la 2018 ni moja ya simu ya bei nafuu kutoka kwa kampuni ya Huawei. Huawei kwa sasa bado wako katika kifungo cha matumizi ya huduma za Google (Google Play Services), app na huduma zingine nyingi za makampuni ya Ulaya na Marekani lakini kwa simu hii bado hali ni tofauti.

Kwa simu ya Huawei Y5 Prime bado hali ni tofauti, simu hii bado inakuja na huduma zote muhimu kutoka kwa kampuni ya Google kama vile app ya Google Play na apps zingine maarufu kama vile Instagram, Twitter, Google Maps na apps nyingine kadhaa muhimu kwa watumiaji wengi duniani.

SOMA PIA  Apple na kufanya iPhone za zamani kuwa nzito, wapigwa faini nchini Ufaransa

Sifa zingine kwa Huawei Y5 Prime

  • Teknolojia ya uoneshi / Graphic card: Mediatek MT6739.
  • Kioo (Display) cha teknolojia ya LCD chenye ukubwa wa inchi 5.45.
  • Mfumo endeshi (OS) wa Android 8.1, EMUI 8.
  • RAM ya GB 2 na diski uhifadhi ya GB 16.
  • Kamera ya Megapixel 13 nyuma na kamera ya megapixel 5 mbele.
  • Betri yenye uwezo wa 3,020 mAh.
SOMA PIA  Vodacom Smart 6: Simu janja ya Bei Nafuu kutoka Vodacom - #Uchambuzi

Simu hii inasapoti teknolojia ya mawasiliano ya 4G ikiwa na huduma nyingine za kimtandao pia kama WiFi na Bluetooth.

tecno

Simu hii pia huja na sehemu ya kuchomeka earphones pamoja na sehemu ya kuchomeka waya wa chaji aina ya microUSB 2.0. ina matoleo matatu ya rangi, Nyeusi (Black), Bluu (Blue) na Dhahabu (Gold).

HuaweiY5Prime2018

Huawei Y5 Prime

 

SOMA PIA  Huawei Watangaza Simu Mpya 'Honor 7i' Yenye Kamera Ya Ajabu!

Simu ya Huawei Y5 Prime ni moja ya simu janja ya bei nafuu yenye ubora wa hali ya juu duniani. Je wewe una mtazamo gani juu ya simu hii? Tuambie kwenye comment.

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania