Katika hali ya ghafla Serikali ya India imetoa agizo la kuzuia mitandao inayoeneza picha, video n.k za ngono kupatikana nchini India. Mara moja watoa huduma wa intaneti mbalimbali wameanza kufuata agizo hilo. Uamuzi huo ambao ukaanza kulaaniwa na wengi mara moja umekuja baada ya maombi ya watu kadhaa kuwepo mahakani tayari kwa muda mrefu ya kupinga upatikanaji wa mitandao ya mambo ya ngono nchini India.
Kupitia mitandao ya kijamii tayari watu wengi nchini humo wameungana katika kupinga uamuzi huo wa serikali ya India kuzuia (ban) zaidi ya mitandao 850 ya kingono ikiwepo maarufu zaidi kama vile PornHub, YouPorn na mingine mingi.
Katika tafiti yetu inaonesha katika wasomaji 10 wa TeknoKona zaidi ya 6 bado huwa wanatembelea mitandao ya namna hii. Piga kura pia katika swali mwishoni mwa makala hii uweze kufahamu kama na wewe upo katika wengi au wachache. 🙂
Wengi wanasema uamuzi huo unaingilia uamuzi wa mtu binafsi huku wakidai hawaoni jinsi mtu anavyovunja sheria au kufanya makosa pale anapokuwa chumbani/nyumbani kwake na kuangalia picha hizo. Wanadai uamuzi huo wa serikali unaingilia haki ya uhuru binafsi wa wananchi ambao unalindwa kikatiba.
Tayari baadhi ya watoa huduma za internet washaanza kufuata agizo la serikali lakini bado wengine wamekataa wakisema watakuwa wanavunja haki za wateja wao. Watafiti mbalimbali wanasema uamuzi wa serikali ata ukifuatwa hautaweza kuwa na nguvu sana kwani watu wanaweza jifunza kutumia teknolojia za maficho kama vile ya VPN ambazo zitawawezesha kutembelea mitandao hiyo bila tatizo huku watoa huduma za intaneti na serikali kutokuwafahamu kabisa.
Wanaounga mkono maamuzi hayo wanadai uwepo wa mitandao hiyo unachangia katika uwepo na ukuaji wa makosa ya kingono kama vile ubakaji
Katika nchi nyingi na ikisemekana Tanzania pia ni mojawapo matumizi makubwa ya kuangalia picha na video mitandaoni huwa utumiaji wa mitandao ya ngono ndio mkubwa zaidi ukilinganisha na matumizi mengine. Na inasemekana uamuzi kama huu uwa unaweza kupunguza mapato kwa makampuni yanayotoa huduma za intaneti kwa kiasi kikubwa.
[socialpoll id=”2256886″]
Mara ya mwisho TeknoKona ilipouliza wasomaji wake kuhusu suala la kuangalia picha/video/mitandao ya ngono wengi walionesha bado wanatembelea kwa sana tuu ingawa ata nchini utazamaji wa mitandao hiyo hauruhusiwi kisheria.
No Comment! Be the first one.