Paka ni moja ya viumbe maarufu sana katika mitandao ya kijamii baada ya binadamu. Na uhakika ushakutana na picha na video kadhaa za paka katika pitapita zako. Kiongozi mmoja wa kidini nchini Saudi apiga marufuku watu kupiga picha za selfi na viumbe hao.
Kiongozi huyo (Cleric) bwana Saleh bin Fawzan al-Fawzan ni mmoja wa wajumbe wa baraza la kidini lenye nguvu sana nchini humo – Saudi Council of Senior Scholars.
Picha/video za paka, na picha za selfi na paka ni maarufu sana mtandaoni.
Bwana Fawzan amesema ‘kupiga picha na paka ni tabia inayosambaa sana kwenye watu wanaopenda kuwa kama wazungu’ (alitumia neno ‘westerners’, yaani watu wa mataifa ya magharibi – Ulaya na Marekani.
Kiongozi huyo aliliongelea jambo hilo baada ya kuulizwa swali kuhusu mtazamo wako juu ya jambo la upigaji picha za selfi alipokuwa anahojiwa katika kipindi cha televisheni.
Baadaye alipanua zaidi tafsiri yake akisema upigaji picha wa aina yeyote kama hauna maana si wa lazima. Alisema isiishiye kwenye paka tuu bali ata na mbwa au kingine chochote kisicho cha ulazima/maana.
@AviMayer Re:Saudi cleric & pictures w/ cats – My personal opinion pic.twitter.com/UiwmmdYYZQ
— Juliana Wagner (@WagnerJwagner23) May 25, 2016
Watu wengi wamejitokeza kwenye mitandao ya kijamii wakipinga katazo hilo, wengi wanaonesha kupinga kwao kwa kupiga picha za selfi na paka wao. 🙂
Je una mtazamo gani juu ya jambo la picha za selfi? Je kunatakiwa kuwa na mipaka (boundaries) katika upigaji picha za selfi?
Chanzo: RT