Ushindani katika makampuni ya simu yanayotumia Android ni mkali sana kwa sababu kuu moja: Kwa kiasi kikubwa wote wanatumia programu ya uendeshaji moja, ANDROID! Hivyo kujitofautisha kuonesha unatoa kilichobora zaidi inakuwa ngumu sana. Tunaona ukichukua baadhi ya aina za LG, Samsung Galaxy, Tecno..unaweza kukuta ukiwekewa kiundani unapata shida kidogo kujua tofauti kuu. Na hichi si kitu kizuri linapokuja suala la ushindani wa kimauzo.
Samsung wanakuletea Galaxy App Store – Soko la programu za simu za Android litakalokuwa spesheli kwa watumiaji wa simu za aina ya Galaxy kutoka Samsung. Katika maelezo yao wamesema baadhi ya programu zitakazokuwa zinapatikana huko zitakuwa zimetengenezwa spesheli kwa ajili ya simu hizi. Hii ni kujaribu kujiweka pembeni na soko maarufu kutoka Google la Google Play.
Watafiti wengi wanaona suala linaweza likaleta matatizo kidogo kati ya Samsung na mlezi mkuu wa programu ya Android – naye ni Google. Kwani katika mikataba ya utumiaji wa matoleo ya Android watengenezaji hawa simu huwa wanakubaliana na Google baadhi ya vitu ikiwapo kuweka programu kuu kama soko la Google Play kwenye simu hizo. Na Google Play ni moja ya sehemu kuu kimapato kwa Google kupitia utengenezaji wake wa Android, na hapa Samsung inaonekana kama nao wanataka sehemu ya ‘mkate huo’ 🙂 .
Ila Google na Samsung wanauhusiano mkubwa sana hivyo suala hili linaweza likawekwa kwenye mazungumzo na labda simu hizo za Galaxy zinaweza zikawa zinakuja na masoko yote mawili, Google Play na Soko la Galaxy App.
Je unadhani suala la kuwa na programu spesheli na soko la kipekee ni kitu kinachoweza kukufanya uchague simu za Galaxy zaidi ya zingine?
Kumbuka kusambaza makala hii, Asante!
No Comment! Be the first one.