Android Wear ni mfumo mpya unaondeleza mfumo wa Android. Mfumo wa Android Wear umebuniwa kwa technolojia za kuvaliwa kama saa-janja (ama kwa lugha ya kigeni: ‘smart-watch’) na miwani-janja ya Google Glass. Ingawa mfumo huu ni mpya, haukubuniwa kuondoa kabisa umuhimu wa simu za mkononi.
Android Wear umebuniwa kupunguza umuhimu wa wewe kutoa simu yako mfukoni kila saa ili kuangalia nini kinachojiri kwenye simu hiyo. Kwa kutumia kifaa cha Android Wear unaweza kubadili muziki, kupokea na kutuma meseji fupi, barua pepe, kunakili, kuweka vikumbusho, kupiga na kupokea simu kufuatilia afya yako na kuangalia apointimenti kwenye kalenda yako.
Saa ya Android Wear ni kama ‘Notification Bar’ yako kwenye mkono ili kukurahisishia maisha ya kawaida, huku ukiwa haujakosa chochote kinachoendelea kwenye ulimwengu wa digitali. Pia, Android Wear ina uwezo wa kuendeshwa kwa kutumia sauti.
Kwa wale ambao wangependelea kupata saa mpya za Android Wear, saa mpya ya LG G watch na Samasung Gear live ndiyo habari ya dunia na zote zimeonekana kwenye Google Playstore wiki hii zikiwa na processor ya 1.2 Ghz na RAM ya 512MB na 4GB za uhifadhi na zikiweza kuhimili kulowa.
No Comment! Be the first one.