Jumapili ilyopita, nchi ya Ujerumani iliibuka kinara wa fainali za kombe la dunia. Kwenye ulimwengu wa mitandao ya jamii hatahivyo, mashindano ya kombe hilo bado hayajaamuliwa kati ya Facebook na Twitter.
Kabla ya kombe la dunia, mitandao yote miwili ilifanya maandalizi ya kuifanya kuwa kitovu cha mazungumzo kuhusu tukio hilo maarufu duiniani. Wiki hii kampuni zote mbili zimeripoti takwimu zikionyesha rekodi zilizovunjwa wakati wa mechi kabambe.
Jumatatu, facebook walitangaza gumzo lililofikia michakato bilioni tatu ikiwemo likes, comments na post kutoka kwa watumiaji millioni 350 huku mtandao wa Twitter ukiripoti ‘tweets’ million 672. Kwa namba hizi, ni wazi kuwa Facebook walishinda kwa kutumiwa zaidi. Hata hivyo, ukichambua zaidi utagundua kwamba Facebook ina watumiaji mara tano zaidi ya Twitter na kwa hiyo, haishangazi kuona utofauti huo wa ripoti wa kampuni hizo mbili. Kwa upande mwingine, ingawa Gumzo kubwa ilikuwa facebook, michakato ya papo kwa hapo, yani ‘laivu’ yalifanyika Twitter.
Wachambuzi wa mambo ya mitandao ya kijamii wanasema kuwa facebook na twitter walijikita kwenye Fainali hizi wakiwa na malengo tofauti. Kwa upande wa Twitter, siku si nyingi zimepita baada ya kampuni hiyo kujifungia kwa wawekezaji. Hofu kubwa iliyojitokeza kwa wawekezaji wa kampuni ni ukuaji mdogo wa watumiaji wapya na uwezo mdogo wa mtandao huo kuwashirikisha watumiaji. Uongozi wa Twitter uliamini kuwa kombe la dunia lingesaidia kuondoa hofu hiyo, japo kwa muda mfupi. Facebook hawana matatizo hayo kwakuwa tayari mtandao huo ni mkubwa kuliko yote duniani. Kwa hali hiyo, kombe la dunia kwa Facebook ilikuwa kujidhihirisha kwa mara nyingine na kuondoa dira ya michakato ya Twitter.
Shayn Patil, mchambuzi wa Wedbush alisema, “Nadhani, Twitter ilihitaji Kombe hili kwa kuzingatia biashara na wawekezaji. Wameamua kujikita kwenye matukio ya ‘laivu’ na hakuna tukio kubwa la aina hiyo mwaka huu zaidi ya Kombe la dunia.”. Zaidi, Patil anaendelea kusema kuwa, “Watu hutumia Twitter kwa muda mfupi papo kwa hapo wakati jambo kubwa linapotokea lakini hawakai. “Mtu anahitaji sababu ya ku-tweet. Baada ya muda anakosa hamasa, anaondoka kwenye mtandao huo.” Pamoja na changamoto zinazowakabili Twitter, kampuni nyingi zimeendelea kuitumia kama inavyoelezwa na Sean Ryan, mkurugenzi wa mitandao ya jamii kwa JC Penney amabye aliuambia mtandao bwa Mashable kuwa wao walijenga mipango yao ya kujitangaza na Kombe la Dunia kwa kujikita zaidi kwenye Twitter.
Kwa kuangalia pande zote mbili, wingi wa watumiaji na gumzo la papo kwa hapo, inaonekana hakuna mshindi wa dhahiri kati ya Twitter na Facebook. Kila moja ina cha kujivunia amabacho ni changamoto kwa mwingine. Jambo ambalo mitandao yote litafurahia ni ongezeko la utumikaji wakati wa mashindano hayo bila kukatika mawasiliano na kupata majanga mengine.
Makala hii imeripotiwa kwa masaada wa Mashable Inc.
No Comment! Be the first one.