fbpx

Roboti kutumika kuwahudumia wazee nchini Japani

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Roboti kutumika kuwahudumia wazee nchini Japani. Serikali ya Japan imeamua kuwa roboti zitatumika kutoa huduma kwa asilimia 80 kwa wazee nchini humo mpaka kufikia mwaka 2020.

Gazeti la “The Guardian” limechapisha habari ya kuwa kiwanda cha roboti nchini Japan kina mpango wa kuboresha roboti ili kurahisisha maisha ya wazee nchini humo kwa kutumia teknolojia.

Roboti kutumika kuwahudumia wazee nchini Japani

Roboti kutumika kuwahudumia wazee nchini Japani

Roboti hizo zitakuwa zikiwasaidia wazee kwa kuwatoa kwenye vitanda hadi kwenye viti vyao na vilevile kuwasaidia kwenye kuoga.

INAYOHUSIANA  Zijue ndege zisizo na rubani zitakazoanza kusambaza madawa Tanzania

Dr Hirohisa Hirukawa, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Robot, Taasisi ya Taifa ya Sayansi ya Juu na Teknolojia amesema kuwa lengo lake kuu ni kurahisisha maisha ya wazee walio katika vituo tofauti na vilevile waliopo majumbani.

Dr Hirohisa Hirukawa amesema kuwa ni asilimia nane ya vituo vya kulelea wazee vinatumia roboti katika kutoa huduma zake.

Vipi je wewe una mtazamo gani juu ya utumiaji huu wa roboti?

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.