fbpx

Nepi janja zipo njiani kuingia sokoni; wenye watoto muwe tayari

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Kutana na nepi janja, nepi itakayokupa taarifa za mubashara kuhusu hali ya nepi ya mtoto 🙂 . Kampuni ya nepi(diaper) ya Huggies ipo katika hatua za mwisho kabisa katika utengenezaji na uingizaji sokoni wa nepi za namna hiyo.

Teknolojia ya bluetooth ndio iliyotumika katika utengenezaji wa mfumo wa mawasiliano kati ya nepi na app itakayokuwa kwenye simu ya mzazi. Nepi hiyo itakuwa na uwezo wa kutuma taarifa kuhusu hali ya nepi ya mtoto.

nepi janja

Nepi ikiwa na eneo la kuscan ili kuweza kuwasilisha data kwenda kwenye app

Huggies hawapo peke yao katika teknolojia zinazofanyiwa kazi katika eneo la nepi za watoto.

  • Kuna kampuni ya Pixie Scientific ambayo tayari inafanyia majaribio nepi zitakazokuwa na uwezo wa kutoa ripoti juu ya afya ya mtoto kupitia mkojo wake.
  • Pia kampuni mama ya Google, Alphabet tayari nao wameshaomba hakimiliki ya teknolojia ya nepi. Nepi itakuwa na uwezo wa kutoa taarifa mbalimbali kuhusu choo cha mtoto, hii ni pamoja ya kufahamu tofauti ya haja kubwa au ndogo.
  • Hata mshindani mkubwa wa Huggies, kampuni ya Pampers nayo ipo katika ubunifu wa nepi zitakazokuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kukausha mkojo.
nepi janja

Tayari kuna makampuni mengi yameanza kuwekeza katika teknolojia zinazohusisha nepi za watoto.

Makampuni ya utengenezaji nepi yamejikuta yakiitaji kuboresha bidhaa zake ili yaweze kuongeza bei kwa kuwa tayari soko la nepi katika mataifa yaliyoendelea kama vile Marekani yanaboromoka. Wateja wanapungua kila mwaka kwa kuwa kiwango cha uzaaji kinaporomoka na hivyo wateja wanapungua.

INAYOHUSIANA  Hatimaye mwanzilishi wa Android azindua simu yake ya Essential

Huggies wanategemea kuingiza sokoni nepi hizo zinazokuja na teknolojia ya bluetooth kufikia mwisho wa mwaka huu kwa kuanza na masoko ya Marekani na Mexico.

Vipi je una mtazamo gani juu ya teknolojia hii ya nepi janja?

Soma makala mbalimbali ya sekta ya afya;
Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.