fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Teknolojia

Ndege ya Milioni 400/= : Hauitaji Mafunzo Kuweza Kuipaisha

Ndege ya Milioni 400/= : Hauitaji Mafunzo Kuweza Kuipaisha

Spread the love

Kampuni moja nchini Marekani imefanikiwa hatua za mwanzo katika nia yao ya kuweza kuingiza sokoni ndege za kutumika kama usafiri wa kila siku kwa watu wa kawaida. Hii inamaainisha hakuna mafunzo makubwa yanaoitajika kama vile ya urubani wa ndege za kawaida.

Ndege hii inayofahamika kwa jina la ICON A5 inatengenezwa na kampuni ifahamikayo kwa jina la ICON lililopo Vacaville katika jimbo la California.icon a5

ukiwasiliana nao na kufanya malipo leo basi utapata ndege yako mwaka 2019

ICON A5 inashika rekodi ya kuwa ndege ya kwanza ndogo na nyepesi itakayozalishwa kwa wingi kwa ajili ya watumiaji wa kawaida. Ni watumiaji wa kawaida kwa kuwa ubunifu na utumiaji wa teknolojia katika ndege hii imeiwezesha kupata kibali cha kuweza kuendeshwa na ata watu ambao hawana leseni ya urubani….ndio kwa kuwa haiitaji mambo mengi kuweza kuipaisha.

Ata 'dashboard' yake ni ya kawaida kama vile uko kwenye gari lolote la kisasa, kilichoongezeka ni kuoneshwa urefu kutoka usawa wa bahari

Ata ‘dashboard’ yake ni ya kawaida kama vile uko kwenye gari lolote la kisasa, kilichoongezeka ni kuoneshwa urefu kutoka usawa wa bahari

Hadi sasa hivi kampuni hiyo tayari inaoda ya ndege zaidi ya 1,500 kwa watu ambao wamekwisha kufanya malipo ya mwanzoni ya zaidi ya milioni 10. Ila ubaya ni kwamba inachukua muda mrefu sana wewe kuweza kupata ndege yako, kwa mfano ukiwasiliana nao na kufanya malipo leo basi utapata ndege yako mwaka 2019.

SOMA PIA  Ifahamu Siku ya Pi (π) Duniani

Kwa wengi waliowahi kuweka oda za ndege hizo wataanza kuzipata kuanzia mwakani mwezi wa saba. Wanasema viendesheo vya ndege hiyo ni virahisi kiasi cha kufanana na uwezo mrahisi wa kuweza kuendesha gari, wanasema inamchukua mtu dakika chache tuu kuweza kujua jinsi ya kuiendesha ndege hiyo.

Ubunifu ulienda kwenye ndege hiyo pia umehakikisha ya kwamba ata kama itilafu ikitokea katika ndege hiyo itaweza kushuka chini taratibu badala ya ghafla ghafla na kwa spidi kubwa kama ndege zingine za kawaida inavyokuwa. Pia kwa usalama zaidi unauwezo wa kufyatua kiti na kuchomoka kupitia teknolojia ya parashuti kwa usalama zaidi pale tatizo linapotokea.maji-ndege-icon-a5

SOMA PIA  Hili ndio toleo la simu janja Oppo Reno6 Pro 5G

Ndege hiyo inauwezo wa kutua kwenye maji au kwenye barabara za kawaida, na kuruka pia kwa kutumia maeneo hayo.

Kazi ipo…. Wenyewe wanadai wanategemea kuuza kwa wingi ndege hizo bila kujali watu wengine wanaoona kama ni teknolojia ambayo muda wake kama bado vileee… Wenyewe wanaamini wapo mabilionea wengi wenye uwezo wa kununua ndege hiyo. Wewe unamaoni gani? Tuambie…

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania