Makampuni mawaili yanayojihusisha na mambo ya wanaanga yanaungana kuhakikisha kwamba yanaleta huduma ya makazi binafsi angani, Bigelow Aerospace pamoja na United Launch Alliance (ULA) watashirikiana ambapo Bigelow watatengeneza nyumba hizo ambazo maalumu kwa matumizi ya angani na ULA watasaidia kuzifikisha katika anga.
Lengo la mradi huu wa Bigelow na ULA ni kuhakisha kwamba wanatengeneza na kuweza kuifanikisha teknolojia ya kupata makazi binafsi katika anga, wanasayansi wanafikiria kupata makazi binafsi angani hasa katika mwezi pamoja na katika sayari ya Mars kwa sababu hizi ni sehemu ambazo binadamu wataweza kuzitumia kwa makazi mbadala wa duniani.
Kampuni ya Bigelow ndiyo ambayo inajishughulisha na utengenezaji wa makazi hayo ambayo yanaweza kukunjwa na kusafirishwa katika ujazo mdogo na pindi yanapofika sehemu ya kutumika yanajazawa hewa na kuanza kutumika. Makazi haya yanawezakutumika angani mwezini ama pia hata katika sayari ya Mars, pia yanaweza kutumika yenyewe kama yenyewe yakielea angani kama setelaiti ama yakiwa yamejishikiza katika kituo cha anga.
Changamoto katika swala la makazi ya huko angani ni kwamba tunataka kitu ambacho kitakuwa ni rahisi kusafirisha kwa roketi kwenda angani, kutoka duniani. Bigelow wamefanikiwa kuitatua changamoto hii kwa kutengeneza kitu ambacho kinaweza kukunjwa na kupunguza ujazo kisha kikasafirishwa na kikifika kinarudia hali yake ya awali kwa kujazwa upepo.
Zaidi ya yote teknolojia hii ya Bigelow inaruhusu hata kwa makazi hayo kuweza kuzunguka dunia kama vile ambavyo satelite hufanya.
Bigelow ndiyo kampuni ambayo ilihusika na utengenezaji wa makazi ambayo yalirushwa na roketi ya Space X kwenda katika kituo cha NASA mwishoni mwa wiki iliyopita.
Kampuni hiyo inasema kwamba imeanza shughuri za kutengeneza makazi hayo na mwaka 2020 itaweza kupeleka angani sampuli moja ya makazi binafsi hayo ambayo itakuwa inaelea huko juu ikiwa imefungwa katika kituo cha kimataifa cha anga na kuweza kuwapatia watu makazi binafsi ila baadaye makazi haya yataweza kupelekwa Mars ama Mwezini ambako watalii wataweza kuyatumia.
Kwa sasa watu ambao wako angani wanaishi katika vyombo vyao huko huko kitu ambacho kinawanyima watu wa kawaida kama watalii kwenda kutembelea anga katika kiasi kikubwa.
Ni ukweli ambao haufichiki kwamba sekta ya utalii wa anga ni moja ya sekta ambazo zitakuwa na mashabiki wengi miaka ya karibuni na ni wazi kwamba makampuni haya mawili yameliona hilo na yanataka kujiwekea nafasi ili kuweza kuvuna faida zaidi. Inategemewa matajiri mbalimbali wataweza kulipia kwenda kuishi kwenye makazi ya namna hii hata kwa wiki au mwezi ikiwa ni aina ya utalii mpya.
2 Comments
Comments are closed.