Kuna mabadiliko yanakuja Twitter ambayo yatawawezesha watumiaji wake kuwa na uwezo wa kuchagua mtu wa kuweza kuchangia kwenye tweet zao.
Uwezo huu unaolenga kuufanya mtandao huo wa kijamii kuwa salama zaidi dhidi ya watu wanaopenda kuacha ujumbe wa matusi, kejeli n.k kwenye akaunti zao bila ulazima wa kuwa’block moja kwa moja – yaani kuwazuia kuona akaunti zao. Utaweza kumzuia mtu kuwa na uwezo wa kuchangia mazungumzo yako tuu, ila abaki na uwezo wa kuyaona.
Ni hivi karibuni tuu Twitter waliweka uwezo wa mtu kuficha baadhi ya majibu/comments kwenye tweet zake. Uwezo huu mpya unaokuja unaenda mbele zaidi.

Baadhi ya watumiaji wa Twitter wategemee kuwa na uwezo wa kufanya haya katika Tweet zao mpya hivi karibuni. Kawaida Twitter ufanya majaribio kwa muda kabla ya kuwapa watumiaji wake wote uwezo huo.
Kwenye tweet mpya utaweza kuchagua watu wenye uwezo wa kujibu (reply) tweet yako kwa makundi haya;
- Global – utaruhusu mtu yeyote Twitter
- Group – Utaweza kuruhusu kundi flani la watu (wanaokufollow tuu au uliowamention/tag tuu)
- Panel – Utaruhusu watu uliowamention tuu kwenye tweet hiyo
- Statement – Hili ni tamko, yaani hakuna mtu yeyote ataweza kujibu tweet yako