Twitter wanawezesha watumiaji wake ku tweet ujumbe wa sauti kwenye mtandao wao maarufu wa kijamii.
Uwezo huo ambao umeanza kupatikana kwa watumiaji wa iOS, yaani iPhone na iPad unalenga kuwapa watu uwezo wa kujieleza kwa njia sauti. Kwa kipindi kirefu ungeweza kutweet kwa njia ya maandishi, picha, GIF au video tuu.
You can Tweet a Tweet. But now you can Tweet your voice!
Rolling out today on iOS, you can now record and Tweet with audio. pic.twitter.com/jezRmh1dkD
— Twitter (@Twitter) June 17, 2020
Je uwezo huo unakuja lini kwa watumiaji wa Android?
Baada ya Twitter kutangaza uwezo huo kwa watumiaji wa iPhone tayari wakaanza kupata malalamiko kutoka watumiaji wa simu za Android wakionesha kutopendezwa na uamuzi wa kuwaacha nyuma.
Twitter hawajasema uwezo huo utakuja lini kwa watumiaji wa Android na pia kwa watumiaji wa Twitter kupitia mtandao (web) ila wachambuzi wengi wanaamini ni kitu kitakachotokea ndani ya wiki kadhaa kuanzia sasa (wiki 2 hadi 5).
Changamoto
Mtandao wa Twitter tayari unachangamoto kubwa ya uchujaji wa jumbe za chuki na ujio wa Tweet za njia ya sauti utaleta changamoto kubwa ya jinsi ya kugundua jumbe za matusi na chuki zinazoweza kuanza kusambaa.
Ujio wa uwezo huu unaweza kupelekea Twitter kuwezesha watu na makampuni ya habari kuweza kuweka vipindi vya Podcast moja kwa moja kwenye mtandao huu maarufu wa kijamii. Kwa sasa unaweza kurekodi ujumbe/tweet ya sauti ya urefu wa sekunde 140 (dakika 2 na sekunde 20).