Baada ya muda mrefu wa kujaribu kuirudisha kwenye chati mwisho umefika, app ya BBM imekufa rasmi. App ya BlackBerry ilikuwa moja ya app maarufu sana na app ya kwanza kuleta uwezo wa kuchati na makundi kwa simu janja – enzi hizo BlackBerry ndio ilikuwa namba moja.
.jpg)
Simu za BlackBerry zilitawala sana katika miaka ya 2007 – 2013, kuchelewa kwa BlackBerry kutumia programu endeshaji ya Android wakati programu endeshaji hiyo imeanza kukua ni moja ya sababu iliyosababisha kuporomoka kwa mauzo na umaarufu wake.
App ya BBM ilianza kupatikana rasmi mwaka 2005, kwa kipindi kirefu ilikuwa inapatikana tuu kwa watumiaji wa simu za BlackBerry. Uamuzi wa kuileta kwenye simu za Android na iOS ulifanyika mwishoni mwa mwaka 2013 ila wakawa wameshachelewa sana kwani apps zingine kama Facebook na WhatsApp wakawa tayari wameshapata umaarufu zaidi.

Tarehe 31 Mei ndio umekuwa mwisho rasmi wa upatikanaji wa toleo la bure kwa watu wote – kuanzia siku hii data zitafutika rasmi.
Nje ya toleo hili kuna toleo la kibiashara la BBM Enterprise – hili litaendelea kuwepo. BBM Enterprise linalenga matumizi ya kikazi zaidi kati ya kundi la watu – kuna mawasiliano ya mmoja mmoja, makundi na vitu vingine vyote vilivyokuwepo kwenye matoleo ya kawaida.
Toleo la BBM Enterprise linapatikana kwa dola 2.49 kwa miezi 6 – takribani Tsh Tsh 7,000 – 8,000, ukipakua unapata muda wa mwaka mmoja bure kabla ya kuanza kulipia.
Anguko la app ya BBM ni kubwa katika historia – kwani ukiwatoa wengine wote bado ni BBM ndio inachukua sifa ya kuwa app ya kwanza ya kuchati kwenye simu katika mfumo wa app ya mtandao wa kijamii. Apps zingine zote kama vile WhatsApp, Facebook na Instagram kuna teknolojia kadhaa wanazozitumia hadi leo ambazo zina historia ya kutokea kwa mara ya kwanza kwenye app ya BBM.