Wiki iliyopita janga kubwa kubwa lilitokea kwa watumiaji simu janja nchini…si kwamba huduma ilikosekana bali mabadiliko makubwa yalifanyika katika vifurushi vya mawasiliano, mabadiliko ambayo kwa kiasi kikubwa yalilenga kuongeza gharama ya huduma ya intaneti.
Walianza Vodacom, na muda si mrefu Tigo wakafuata, kabla hali haijatulia Airtel nao wakafanya mabadiliko pia. Je sababu ni nini? Endelea kusoma
Hatukuandika kwa haraka kuhusu ila tukaamua tufanye utafiti zaidi na hii ikiwa na kusubiri kupata habari ya undani kutoka kwa vyanzo vyetu vilivyo katika makampuni husika.
Je ulikuwa ni uhamuzi wa pamoja?
Hapana, inaonekana ni uhamuzi ambao ulianza Vodacom lakini wengine wakaamka na kufanya hivyo kwani kiuhalisia wote hawakuwa wanafaidika kutokana na ushindani wao uliofanya bei ya data/intaneti iwe moja ya chini kabisa duniani. Huu unaonekana na uhamuzi wa kibiashara zaidi tena wa kimaslahi ya kutaka kuongeza mapato.
Chini kabisa duniani?
Ndio, uwezi kuamini kwa kipindi kirefu tulikuwa tunalipia data kwa bei ghari, lakini mambo yalibadilika kutokana na ukuaji wa ushindani na upatikanaji bora wa intaneti kiasi cha kufanya bei kushuka kwa kasi. Kwa kipindi kirefu kabla ya wiki iliyopita tumekuwa tunatumia intaneti kwa gharama nafuu zaidi katika ukanda mzima wa Afrika mashariki.
Moja ya taarifa kutoka ndani ya moja ya kampuni hizo kubwa alituambia kwa kimombo;
“We have been locked in a price wars. Which have driven the price of data practically below cost” – Chanzo chetu
Utafsiri wa haraka haraka -> “Tumekuwa tumejibana katika ushindani wa bei kwa muda mrefu. Ushindani huo ukasababisha kufikia hali ya kutopata faida baada ya kutoa gharama za uendeshaji”
Ahadi ya mkongo wa intaneti wa taifa kuleta intaneti nafuu vipi?
Wengi wetu tulikuwa tumechukulia unafuu wa bei tulikuwa tunaufurahia umetokana na pesa chungu nzima zilizotumika kwenye kujenga miundo mbinu ya intaneti ya fiba nchi nzima. Vyanzo vyetu vya ndani vinadai si kweli miundo mbinu hiyo imeleta unafuu wowote kwani bado inawabidi kugharamia teknolojia mbalimbali katika kutumia huduma hizo hivyo bado hakuna tofauti yeyote.
JE BEI ITAENDELEA KUWA KUBWA?
Biashara ni ushindani, TeknoKona tunaamini bado kuna uwezekano wa bei kushuka kidogo, ata kama si kama zamani. Mabadiliko yaliyofanyika ni ‘extreme’, yaani wamefanya makubwa sana na yanairudisha Tanzania nyuma katika ukuaji wa moja ya huduma muhimu sana kwa sasa katika mawasiliano. Labda ushindani utaendelea na tutegemee mambo kuwa mazuri…..na kuna mtandao mpya upo njiani kuingia tena kinguvu zaidi kwenye suala la data/intaneti, namaanisha Viettel. (Soma kuhusu Viettel – HAPA)
Utakuwa ushasikia sababu mbalimbali kutoka kwa watu lakini ni ukweli usiopingika huu ulikuwa uhamuzi wa kibiashara zaidi, na siko zote huwa unakuwa wa kifaida zaidi…hasara kwetu watumiaji. 🙁 Tunategemea kuona kampuni moja moja kujaribu kuongeza ongeza kidogo ili kuzidi kuwa juu ya wenzake, na hapo ndio unafuu utajitokeza.
Nini ufanye kwa sasa kupunguza utumiaji wa data?
- Ni muhimu ukumbuke kujiunga bando za intaneti tupu kama wewe ni mtumiaji wa simu janja yenye apps nyingi kama Whatsapp n.k.
- Ondoa chaguo (setting) ya apps kushushia ‘updates’ yenyewe, kuondea angalia ‘settings’ ndani ya app ya Google Play kama unatumia Android.
- Kwenye WhatsApp unaweza zuia picha na video kutoka kwa watu kujishusha (download) bila idhini yako. Bofya HAPA kujua jinsi ya kufanya hivyo.
Je umeathirika sana na mabadiliko haya? Tueleze kupitia akaunti zetu Twitter, Facebook na Instagram ,pia unaweza jiunga nasi kwenye swali letu Facebook ambapo watu wanazungumzia mabadiliko haya – Bofya HAPA!
No Comment! Be the first one.