fbpx

Maana ya “TTY Mode” kwenye rununu

0

Sambaza

Simu tunazonunua zina vitu vingi ambavyo si rahisi kuvifahamu kwa mara moja au tusifahamu kabisa tusipokuwa watu wa kupenda kujua mambo mengi kwenye vifaa tunavyomiliki na moja kati ya vitu hivyo ni maana ya “TTY Mode” kwenye rununu.

Teknolojia inakua kila uchwao ikitoa tafsiri kwamba watu wanabuni namna ambavyo kitu watakachokileta kitasaidia makundi yote ya watu na kadri siku zinavyosogea ile dhana ya kwamba kundi fulani limesahaulika inapotea, nitakwambia kwanini.

“TTY Mode” au “Tele Type Writer/Text Telephone” ni mfumo wa simu ambao unasaidia watu wenye ulemavu wa kusikia au matatizo ya kuongea kuweza kuelewa kitu kilicho katika mfumo wa sauti.

kwenye rununu

Simu yenye uwezo wa kutafsiri sauti na kuweka katika maandishi mahususi kwa walemavu wa kusikia au matatizo ya kuongea.

Sasa kwenye simu janja mbalimbali (LG, Samsung, n.k) unaweza kuwa umeshakutana na kipengele hicho ukawa unajiuliza “Kina kazi gani?”. Kwa kuwa umeshafahamu kuwa kinasaidia/ni mahususi kwa wale ambao wana matatizo ya kusikia/kuongea ni vyema ukatambua kuwa  iwapo ukiruhusu kipengele hicho basi huduma kama ujumbe mfupi wa maneno, kuelewana na mtu akikupigia vinaweza visifanye kazi vyema.

kwenye rununu

Namna ya kuruhusu au kuzuia kipengele cha “TTY Mode” kwenye rununu.

Hivyo ndivyo teknolojia inavyosaidia hata makundi yenye mahitaji maalum ingawa inawezekana kabisa ni kundi dogo tu la walengwa ndio wanaofahamu kuhusu jambo hilo. Usisite kushirikisha na wengine.

Vyanzo: Tech Junkie, Tech Walla

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Simu janja ya kwanza yenye "V" mbili
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.