Kusoma vitu kwenye mtandao kwa kutumia kompyuta ni kitu cha kawaida sana na kuna wakati unataka uweze kuutunza ukurasa fulani wenye habari ambayo unataka kuja kuisoma baadae lakini inakuwa changamoto kidogo kwako.
Unaweza ukafikia uwamuzi wa kutafuta mtaalam wa masuala ya kompyuta au mtu ambae ni mtundu mtundu kwenye kompyuta ili akusaidie kuutunza ukurasa wa kwenye tovuti fulani kwenye kivinajri. Huhitaji msaada wa mtu yeyote isipokuwa wewe mwenyewe tu!
Namna ya kutunza ukurasa kwenye kivinjari.
Kama wewe unatumia kivinjari mara kwa mara (iwe kwenye simu/kompyuta) utakuwa umeshaona alama ya nyota/kopa upande wa kulia kabisa kwenye uwanja wa kuandika tovuti. Basi leo fahamu ya kuwa ukibonyeza kitufe hicho (alama ya nyota/kopa) utakuwa umeuhifadhi ule ukurasa bila kunakili jina la tovuti kwa ajili ya wewe kukumbuka hapo baadae.

Jinsi ya kutafuta ukurasa uliouhifadhi.
Inawezekana umetunza lakini sasa hujui namna ya kuupata ule ukurasa ambao uliutunza wakati fulani kwa lengo la kutaka kuutembelea wakati wowote utakapohitaji na njia rahisi na kamwe haitakusumbua ni kubonyeza CTRL+SHIFT+B (kwenye Windows) au Alt + ⌘ (kwenye kompyuta za MAC).

Kwa wanaotumia kompyuta za MAC inaweza kuwa rahisi zaidi kupata kurasa walizozihifadhi.

Hii inamaanisha hakutakuwa na haja tena ya kufungua kurasa nyingi kwenye kivinjari kisha kutozifunga baada ya kumaliza kusoma/kufanya kitu kingine kwa hofu ya kuupoteza ukurasa husika.
Vyanzo: Opera Blogs, Mitandao mbalimbali