fbpx

Umemiss Windows 95? Unaweza kutumia Windows 95 ndani ya Windows 10, MacOS au Linux

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +

ICT CONFERENCE 2019

Sambaza

Kwa wale ambao walifanikiwa kutumia kompyuta miaka ya mwishoni ya 90 na mwanzoni wa miaka 2000 basi kompyuta ya kutumia ilikuwa ni inayotumia programu endeshaji ya Windows 95.

Windows 95 ilitolewa rasmi tarehe 15 Agosti mwaka 1995 na ndio toleo la Windows lilibadilisha kabisa mfumo wa programu endeshaji na kufanya kompyuta kuwa rahisi zaidi kutumiwa na watu wa aina mbalimbali.

INAYOHUSIANA  'Kusave' Maifaili ya WhatsApp kwenye Memori Kadi! Je inawezekana?

Toleo la Windows 95 ndio lilitambulisha vitu vipya kwenye Windows ambavyo vinatumika hadi leo, hii ni pamoja na Taskbar, Start Menu, na muonekano mzima wa programu endeshaji ya Windows (GUI).

windows 95 muonekano

Muonekano wa WIndows 95

Kama unataka kukumbuka miaka hiyo ya nyuma au kuna viprogamu unaitaji kuchunguza zilivyokuwa zinafanya kazi basi kuna mtafiti mmoja amefanikisha kufuma toleo la Windows 95 ndani ya programu spesheli ya ‘Virtual’ inayowezesha Windows 95 itumike kama app au programu nyingine yeyote.

INAYOHUSIANA  Jinsi ya kusambaza kitu chenye ujazo mkubwa kwenye WhatsApp #Maujanja

Utaweza kuipakua kwenye kompyuta inayotumia Windows 10, Linux au MacOS na kisha kuitumia kwa urahisi tuu.

Faili la kudownload lina ukubwa wa takribani MB 300 na ukishapakua (install) litakuwa na ukubwa wa kati ya MB 500 hadi GB 1.

Windows 95 hii inakuja na programu mbalimbali
– Microsoft FrontPage, Netscape 2.0 na FrontPage Server
– Magemu kama vile Doom, Wolfensterin 3D, A10 Tank Killer na Grand Prix Circuit.

INAYOHUSIANA  Yandex.com - tovuti mbadala ya utafutaji kwa Google.com

Unaweza kupakua Windows 95 kupitia tovuti ya GitHub – Windows 95

Facebook Comments

Sambaza

ICT CONFERENCE 2019

Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.