Ni wazi kwamba hakuna anayependa kununua simu janja ambayo ni feki kwani inaumiza sana pale unapotumia hela nyingi kununua simu nzuri ukidhani ni orijino alafu unakuja kugundua ni feki.
Tecno wao wamejidhatiti kwa kuhakikisha simu zao zinajulikana kwa urahisi iwapo ni feki au si feki na ni nadra sana kusikia Tecno wakilalamikia walanguzi wanaotengeneza simu feki zenye jina la Tecno. Ni Nigeria tu ndipo ambapo Tecno wamekubana na simu feki zenye jina la Tecno.
Nawezaje kujua iwapo Tecno yangu au betri lake ni feki au la?
Ni hatua chache lakini muhimu sana ambazo zitakuwezesha kujua iwapo simu yako aina ya Tecno ni feki au halisi. Fuata hatua hizi na utajua tu kama Tecno yako ni ‘yenyewe’ au feki.
- Nakili IMEI na VC namba ambazo zimebandikwa kwenye boksi lilikuja na simu yako.
VC namba ipo pembeni tu ya IMEI namba na zinaweza kuwa zimebandikwa juu, pembeni au upande wa chini wa boksi la simu yako. Kama unaangalia kuhusu betri basi andika namba ya SN iliyokwenye betri husika.
2. Tembelea tovuti ya Tecno mahususi kwa ajili ya kujua iwapo simu/betri ya simu yako aina ya Tecno ni halisi au feki. – http://gc.tecno-mobile.com/
Kisha ingiza namba husika (IMEI na VC namba) kuweza kuja iwapo simu janja yako ni yenyewe au la! IMEI namba ina tarakimu 15 huku VC namba ina tarakimu 6. Kwenye betri angalia kitu kinaitwa SN…kuna namba mbele yake.

3. Utapata majibu iwapo betri au simu janja yako ya Tecno ni orijino au ni feki
Baada ya kubonyeza kituufe kilichoandikwa ‘Submit‘ na kusubiri kwa sekunde kadhaa ukurasa wa tovuti ambayo ni maalumu kwa ajili ya kuhakiki kama simu yako aina ya Tecno itafunguka na kurejesha majibu; iwapo simu hiyo ni OG au la!

Ni muhimu sana kununua simu kutoka kwenye maduka amabayo yamepewa mamlaka ya uuzaji wa simu kutoka kwa kampuni husika ili iwe rahisi wewe kupewa msaada kuhusiana na simu yako pale inapopata tatizo/kama sio halisi uweze kuirejesha na kupewa simu nyingine.
Je, nini maoni yako kuhusiana na hiki tulichowaeleza? Tuambie katika sehemu ya comment hapo chini.
Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTube, Telegram na Google Plus
Vyanzo: Dignited, jalingo.co