fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Android iOS Operating System Teknolojia Windows Windows Phone

Kaspersky: Windows Ndio OS Bora Kuliko iOS, OS X, Na Android!

Kaspersky: Windows Ndio OS Bora Kuliko iOS, OS X, Na Android!

Spread the love

Mmiliki na muanzishi wa kampuni ya IT inayojihusisha na usalama ya Kaspersky Bw. Eugene, amesema katika  mkutano wa kiusalama wa AusCERT kuwa Windows ndio programu endeshaji bora kulinganisha na iOS, OS X, na hata Android huko nchini Australia.

Mtaalamu huyo wa mambo ya kiusalama wa kompyuta na simu pia amesema kuwa Windows wameonyesha ubora wa hali ya juu kwani wanajitahidi katika kuboresha usalama wa programu endeshaji (OS) yao.

Microsoft wamekuwa wakifanya jitihada za nguvu juu ya kuangalia ni namna gani wanaweza kuzuia mashambulizi mengi na kuboresha ulinzi wa watumiaji wa Os zake hasa katika hii inayokuja ya Windows 10. Eugene na kampuni lake la kiusalama anachambua zaidi ya 300,000 ya ‘Malwere’ kwa siku, Kampuni limekuwa likiboresha njia ya kisasa ya kujikinga na vitisho ambavyo vinaweza vika athiri kompyuta kwa dunia.

Nembo Ya Kaspersky

Nembo Ya Kaspersky

Kampuni imekua ikikusanya taarifa kwa watu milioni 400 ambao ni watumiaji wa kudumu wa kaspersky kuhusiana na sampo za malware na virusi vya aina mbalimbali ili kuona ni OS (operating system) gani ambazo ni dhaifu na ni rahisi kwa watu ku ‘hack’

Benki za kwenye simu zimejulikana kwa kiasi kikubwa cha matukio ya wizi kutokana na watu wengi kuhamia kwenye simu (e-mail na mitandao ya kijamii) katika kufanya miamala yao ya kila siku. Kaspersky wamekuwa wakitoa suluhisho la namna yake —”disconnect from the Internet”— yaani jitoe katika intaneti  na hii ikiwa na kinga kwa vifaa vyote

Bwana Eugene pia alisema pia alisema kuwa  hana simu janja na pia amekuwa akitumia  akitumia sonny ericsson ya kizamani kwa ajili ya mawasiliano.

Bwana Eugene

Bwana Eugene

Kaspersky walisema kuwa siku hizi Antivirisi sio kama zamani jinsi zilivyokuwa zinafanya kazi  ya kuzui virusi tuu bali kuna mambo mengi ndani yake siku hizi kama vile uhalifu wa kimtandao, hujuma, upelelezi na kadhalika

SOMA PIA  WhatsApp Web Beta (toleo la majaribio) lawezeshwa kuweza kuficha jumbe za watu

Alisema hata kama ni vigumu sana kuzindua ‘malwere’ katika  system ya  iPhone  kwa sababu OS yake imefungwa kwa watu wa nje wa masula ya programing. Kila System ina mapungufu yake na hiyo inaifanya iPhone kuwa na mapungufu makubwa sana katika simu janja. Kitu kibaya kinachoweza tokea ni kama mamilioni ya iPhone yata vamiwa kiusalama, basi tiba haitapatikana haraka kwa kampuni la Apple haliruhusu wataalamu wa nje wa ‘programming’  katika system zao hiyo itapelekea makampuni mengi ya kutengeneza Antivairasi kushindwa kufanya kazi.

Kuhusu Android, Kaspersky wamesema kuwa kutokana na kwamba ni maarufu na ni ‘system’ ambayo iko wazi itakuwa ni rahisi sana kutatua mshambulizi. Kwa mfano hebu fikiria Android imepatwa na majanga (mamia ya simu) itakua ni rahisi kupatia tiba tatizo hilo kwa Android ipo wazi karibia kwa kila mtu. Watengenezaji wa antivairasi hawatapata shida katika kutengeneza kinga.

SOMA PIA  Sifa za kuvutia wateja zinazoihusu Tecno Camon 18T

Cha kufurahisha ni kwamba Kaspersky wemeitaja Os ya Windows kuwa ni Os (Katika simu) kuwa ni ile ambayo iko safi kabisa. Na hii ni kwa sababu njia ya usalama katika simu unaotolewa na Microsoft ni ule wa hali ya juu kama ule unaotolewa na Apple.

iOs na Android zina simu nyingi sana sokoni kulinganisha na zile za windows na hii inaonyesha hata likitokea tatizo (Shambulio/virasi) basi simu za windows hazitaumia sana. Je wewe mwana TEKNOKONA unaona hii ni sawa? Windows iko juu ya iOS na Android? Dondosha comment yako hapo chini

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania