Teknolojia inazidi kukua! Watafiti kutoka chuo cha Columbia cha nchini Marekani wamefanikiwa kutengeneza kamera ya kwanza duniani yenye uwezo wa kufanya kazi bila kutumia vyanzo vya kuchaji na ikaweza kufanya kazi upigaji picha usiokwisha.
Je nini hasa wamekifanya?
Watafiti hao wameweza kutumia sensa ambazo zipo kwenye kamera hizo hizo kuwa na uwezo wa kufua umeme kama vile teknolojia inayotumika katika umeme wa jua (Solar), baada ya kufua umeme huo mdogo, ndiyo unatumika katika ufanyaji kazi wa kamera hiyo.
Profesa Nayar anayeongoza timu ya ugunduzi huo amesema wazo ilo lilikuja pale alipogundua teknolojia inayotumika katika kutengeneza vioo vya kufulia umeme wa jua (solar panels) na ile teknolojia ya ndani ya kamera za kisasa zinafanana sana. Kitu kikubwa sana kinachotumika kote kinafahamika kama ‘Photodiode’, na wakafanikiwa kukifanya kifaa hicho kiweze kusensi mwanga kama vile kinavyotumika kwenye kamera na pia wamewezesha kifaa hicho kuweza kubadilisha mwanga unaopokelewa kwenye kwenye nguvu ya umeme kama vile teknolojia hiyo inavyotumika katika ‘solar panels’.
Katika kamera hii waliyofanikiwa kutengeneza wametengeneza kifaa hicho kwa pixels ndogo za 30 kwa 40 tuu na hivyo picha zake zipo za kiwango kidogo na ni si za rangi. Kuonesha uwezo wa kifaa hicho tayari timu hiyo imeonesha picha na video walizofanikiwa kurekodi kwa kutumia kamera hiyo.
Je teknolojia hii itaingia sokoni?
Timu hiyo ipo makini sana katika kuhakikisha teknolojia hii inakua na kaisi cha kuweza kutumika haraka iwezekanavyo katika vifaa vingine kama vile kamera za ulinzi, simu janja na ata kwenye vifaa vingine vyenye kamera.
Tayari wanampango wa kutengeneza kamera yenye nguvu zaidi na ya kisasa kutokana na kile ambacho wamejifunza kutokana na mafanikio yao katika kutengeneza hii ya kwanza.
Kuna sehemu nyingi sana teknolojia hii inaweza kutumika.
- Inaweza ikawekwa kwenye simu janja na hivyo kuondoa kabisa utumiaji wa betri la simu kwa ufanyaji kazi wa kamera,
- pia njia nyingine ya kutumika ni pamoja na kuwezesha simu zetu janja zenye kamera kuweza kujichaji zenyewe kupitia kamera zake.
- Na kwa kamera za ulinzi basi inamaanisha zitaweza kufanya kazi bila kuitaji chanzo kingine cha umeme
Kwenye mfano wao, yaani ‘prototype’ kamera hiyo inaonekana kubwa lakini Profesa Nayar anasema ni kitu rahisi na kinachokuwa cha gharama ndogo kutengeneza kifaa hicho kwa udogo mdogo wa sifa ya kuitwa ‘chip’ kama vile sehemu ndogo ndogo za ndani ya simu yako.
Mambo ndiyo hayo, habari nzuri zinazidi kuja katikaeneo la teknolojia ya kuchaji na betri. Kumbuka kwa miaka mingi teknolojia nyingi sana zimeweza kukua kwa haraka katika maeneo ya simu na kamera lakini ni teknolojia ya betri ndiyo imekuwa inaukuaji mdogo sana na hivyo kuathiri raha ya kutumia vifaa vyetu hivi vyenye uwezo mkubwa.
Endelea kutembelea mtandao wako namba moja kwa habari na maujanja ya Teknolojia! Kumbuka kusambaza habari na maujanja kwa ndugu na marafiki!
Soma Pia: Betri Inayojaa ndani ya Sekunde 60!
No Comment! Be the first one.