fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Android

Jinsi ya Kuongeza Nafasi Kwenye Simu Yako ya Android

Jinsi ya Kuongeza Nafasi Kwenye Simu Yako ya Android

Spread the love

Kama ni mtumiaji wa simu za Android (kama mimi) lazima umekwisha kutana na jambo hili. Mara kwa mara simu yako itakupa ujumbe kuwa imejaa. Kinachosababsha simu yako kujaa mapema si simu bali ni program (applications) unazopakua na kutumia pia maudhui kama vile picha, muziki na video.

Je unawezje kuongeza nafasi kwenye simu yako ya Android? Tutatumia mfano wa Huawei Y360. Sababu ya kutumia aina hii ya simu kama mfano ni kwa vile inaaminika na kupendwa na watu wengi, japo ni simu mpya hapa nchini lakini wengi wanazipenda na wanaendelea kuzipenda. Mara kwa mara nikitembelea maduka ya Tigo (zinakouzwa kwa shilingi 160,000 pekee) hukuta foleni za watu na wahusika huripoti kuwa ndizo habari ya mjini kwa sasa.

Huawei Y360

Huawei Y360

Jinsi ya kuongeza nafasi kwenye simu yako ya Huawei Y360

Futa programs ambazo huzihitaji. Nenda Settings >> All (Juu kulia) >> Apps kisha futa program ambazo huzitumii.

Clear App Cache’ Nenda Settings >> All (Juu kulia) >> Apps, kisha chagua program ambazo zinachukua nafasi nyingi (Mara nyingi huwa Instagram na Whatsapp) kisha bonyeza mahali palikoandikwa Clear Cache

SOMA PIA  Kati Ya Pin Na Pattern, Kipi Bora? #Android #Usalama

Hamishia programu zako kwenye memory card. Huawei Y360 huja na internal memory ya 4GB ila unaweza kuweka memory card hadi ya 32GB. Kuhamishia program zako kwenye memory card kutasaidia sana kuongeza nafasi kwenye simu yako.

Soma Pia – Apps Mbili Bomba kwa Ajili ya Ku-uninstall Apps Nyingi Kwa Mkupuo Kwenye Android!

Tumia Master cleaner.  Huawei y360 huja na program maalumu iitwayo Master Cleaner. Hii itakusaidia kudelete mafaili ambayo huyahitaji kwenye simu yako na kukuongezea nafasi zaidi.

SOMA PIA  Jinsi ya ku-convert Mafaili Yoyote kwenda Mfumo wa PDF kwenye simu za Android

Soma Pia – Clean Master: Moja App Muhimu Kuwa Nayo

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania