fbpx

Rais Trump airudisha ZTE Marekani kufanya biashara

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Rais Donald Trump wa Marekani amesema kwa njia ya Twetter kuwa Marekani na Uchina zinafanya juhudi kuifanya kampuni ya ZTE ya nchini Uchina irudi kwenye biashara yake, baada ya kupigwa marufuku nchini Marekani.

Rais Trump amechapisha kupitia akaunti yake ya Twitter kwamba pande hizo mbili zinafanya kazi kwa pamoja ili kutafuta njia ya kuifanya kampuni ya ZTE irudi kwenye biashara yake haraka na kuongeza kuwa ameiagiza wizara ya biashara ya Marekani ikamilishe kazi hiyo.

Inakadiriwa kuwa kupigwa marufuku kwa kampuni ya ZTE kumeleta hasara kwa kampuni za Marekani kwenye mapato yake hususani zile zinazouza bidhaa kwa ZTE na kupunguza kwa nafasi za ajira kwa watu kadhaa.

Rais Trump airudisha ZTE Marekani

Ujumbe wa rais Trump kwenye Twitter akizungumzia suala zima la kuirudisha ZTE kufanya bishara Marekani.

Kwanini ZTE ilifungiwa?

ZTE walipewa adhabu ya kutofanya biashara nchini Marekani kwa muda wa miaka saba baada ya kubainika kuwa ilikuwa inafanya biashara na Korea Kaskazini pamoja na Iran wakati wa utawala wa rais Obama.

Vilevile, Marekani ilizuia bidhaa za ZTE na Huawei kwa wananchi wake kutozitumia kwa sababu haziamini. Ushauri huo ulitolewa na viongozi wa juu wa mashirika ya kipelelezi ya CIA, FBI na NASA. Hata hivyo, katazo hilo lilionekana lipo kwenye ushindani wa kibiashara unaotishia soko la bidhaa za Marekani kutoka kwa zile za Uchina.

Rais Trump airudisha ZTE Marekani

ZTE tempo Go; Moja ya bdhaa za ZTE (kampuni).

Kuondolewa kwa adhabu waliokuwa wamepewa kampuni ya ZTE na mamlaka husika inamaanisha kuwa kampuni za kutengeneza vipuri kama prosesa za Qualcomm zitakuza kipato chao kwani ZTE ni moja ya wateja wa kubwa wa vipuri hivyo.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Programu ya usaidizi kutoka Google kutanua wigo wake
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.