Android ni moja ya mfumo maarufu zaidi duniani wa kuongoza simu, ikiwa imeunganisha kampuni nyingi na kubwa sana za kutengeneza simu janja.
Simu janja kutoka Samsung, Sony, HTC, Huawei, Tecno, sasa hata baadhi ya Nokia au Blackberry zinatumia mfumo huu, japo kwa matoleo tofauti kulingana na uwezo wa simu.
Lakini ukubwa wa mfumo huu wa simu janja duniani, hakujazuia mfumo huu kuweza kuwekwa na kutumiwa katika Kompyuta za kawaida. Kuna namna tofauti za kutumia mfumo huu kwenye kompyuta, kama kutumia Kifaa Maalum Cha mfumo wa Android kwenye kompyuta yako, Kuweka mfumo wa uendeshaji (OS) wa adroid kwenye kompyuta yako au kutumia App maalum.
Hii ina maana kuwa, ukiwa na mfumo wa Android kwenye PC yako, utakuwa na uwezo wa ‘Kuinstall’ na kutumia App na Game zote zinazopatikana kwenye Playstore katika PC yako. Ndio. Tuangalie Njia moja baada ya nyingine upate maujanja zaidi.
Kwa Kutumia App kama Vile BlueStacks
Njia hii ndio rahisi, na yenye faida zaidi kwa watumiaji wa kawaida. Kutumia app kuendesha mfumo wa android kwenye PC yako ni rahisi kwa sababu unahusisha Mfumo wako unaotumia kwa wakati huo (Windows 7, 8, 8.1, au 10). App kubwa na inayofanya kazi vizuri zaidi ni BlueStack.
Ilianzishwa mwaka 2011 kwa ajili ya kuunganisha mfumo wa android kwenye PC yako. Ukiwa na BlueStack, mtumiaji unaweza kudownload App na Games mbalimbali kutoka PlayStore, au Amazon AppStore kusha kutumia App hizo katika PC yako.
Ukishusha mfumo wa BlueStack, utapata Toleo la 4.4.2 KitKat la Android. Japo ni matoleo mawili nyuma ya mfumo wa sasa, lakini kuna dalili za kuletwa Masasisho ya App hii maarufu sasa kwa watumiaji wa PC.
Japo ina kasoro zake, mfano kucheza baadhi ya michezo ya 3D, au baadhi ya michezo ya 1080p kwa kushindwa kuchezesha vivuli n.k. Lakini watumiaji wanafurahia huduma nyingine muhimu za App kama Whatsaap, Instagram na Games. Vyote vilivyo PlaStore. BlueStack pia inakuwezesha kuhamisha mafaili kama yale ya APK kutoka kwenye komputa kwenda kwenye simu ya Android.
Ni mfumo mzuri, na mrahisi kutumia kama ni mara ya kwanza kuanza ujanja huu. Unaweza ukaudownload kwenye PC yako kwa kubonyeza HAPA
Kwa Kutumia ‘Remix OS’
Japo ni jina geni katika ulimwengu wa Android, lakini ni mwanzo wa safari ndefu Kampuni Ya Remix OS imemeanza kuja nayo kuwafikia wapenzi wa Android. Remix OS inawapa watumiaji wake kitu ambacho wengi hawakipati, ‘Multitasking’. Uwezo wa kifaa chako kufanya kazi tofauti kwa wakati mmoja.
Uki ‘Install’ mfumo huu kwenye kompyuta yako, utaweza kupata mwingiliano mzima wa mfumo wa Android, ukiwa na sehemu ya ‘Task Bar’ na sehemu za App. Kwa sasa kuna namna moja tu ya kuhifadhi mfumo huo katika PC yako, na ni kwa kutumia ‘Bootable USB Drive’. Kuna matoleo tofauti kulingana na baadhi ya PC. Ukihifadhi mfumo huu kwenye PC yako utaweza kuhifadhi na Google PlayStore, na unaweza kudownload App zote za Adroid kwenye PC yako.
Kumbuka kwamba mfumo huu ni wa majaribia ya mwanzo kabisa, hivyo tegemea kukwama kwama kwa hapa na pale, matatizo ya kiufundi yasiyoeleweka. Nashauri kutumia Mfumo wa kwanza, ila kama unapenda maujanja, jaribu utushirikishe uzoefu wako. Unaweza ipata hapa -> Remix OS
Kwa kutumia ‘Virtual Device’
Google wanakupa ‘Official Andoid Emulator’ ili kukuwezesha kuendsha mfumo wa Android kwenye kompyuta yako. Hii inakupa uwezo wa kila kitu wa mfumo wa android katika PC yako. Imetengenezwa kwa ajili ya kukidhi haja ya wataalam na wategenezaji wa Android Apps.
Japo iko taratibu, lakini ina faida nyingi wa watengenezaji hasa wakati wa kufanyia majaribio App ambazo zipo tayari kupakiwa katika App Store.
Bahati mbaya, Emulator hii iko pole pole sana na haipendekezwi kwa matumizi ya kila siku. Pia hauji na Google PlayStore. Kama Hakuna Playstore, inamaanisha kuwa hutakuwa na uwezo wa kuhifadhi App mpya bila kuwa na utaalamU mbadala wa kufanya hivyo.
Kama wewe si mtengenezaji wa App, kuwa na Virtual Device katika kompyuta yako kunaweza kuwa sawa na kupoteza nafasi tu kwenye PC yako. Mfumo huu unafanya kazi kwenye OS X, Windows na Linux.
Kila mfumo unafaida zake na hasara zake. Inategemena na wewe unataka kwa matumizi gani katika Desktop ya Kompyuta yako. Kama wewe ni Mbunifu wa App, basi Virtual Device kama vile AVD Manager itakuwa chaguo bora kwako.
Kama unataka kutumia Android kwenye kompyuta yako kama unavyotumia Simu yako, basi BluStack ni ya kwako. Remix OS ina mengi ya kukupa japo bado ni mfumo mchanga sana na mgumu kutuumia. Masasisho yake siku za usoni huenda yakawa tishio Sokoni.
Kuwa mtundu, usiogope kujaribu kama unataka kuwa mjanja, jaribu zote, kisha tuambie ipi inafaa zaidi kwako.
Chanzo cha Makala haya ni DigitalTrend na Android Authority
No Comment! Be the first one.