
Ni wazi kabisa kuna njia nyingi sana za kufuta mafaili katika kifaa cha iPhone na iPad–na pia sababu za kufanya hivyo ziko nyingi tuu inategemea kwa mtu na mtu.
Kuna wengine wanafuta mafaili hayo ili waweze kupata ujazo mwingi wa uhifadhi katika simu ya iPhone , iPad au pengine mafaili hayo hayana matumizi tena –sababu ziko nyingi.

App Ya Files Katika iPhone
Njia rahisi ya kufuta mafaili hayo moja kwa moja ni kwa kutumia huduma ya Files ambayo Apple kwa mara za kwanza kabisa waliitambulisha mwaka 2017.

App Ya Files Katika iPad
Files inawasaidia watu wanaotumia iPhone kuweza kuhifadhi na kufikia mafaili yao kwa urahisi kabisa na kingine kikubwa ni kwamba mtu unaweza unganisha moja kwa moja huduma hiyo ya mafaili na iCloud.

Muonekano Wa App Ya Files
Kwa kutumia App hii unaweza ukaingia na kuangalia vitu mbali mbali vinavyokula ujazo wa uhifadhi wa iPhone yako bila kutumia App zingine kutoka kwa watu wengine (sio Apple).

Moja Kati Ya Huduma Za Ujazo Uhifadhi Wa Mtandaoni Katika App Ya Files
Kwa kutumia huduma hii ya Files utawezesha kufanya jambo hilo (kufuta) mafaili mbali mbali kulingana na sababu zako. Kama nilivysoema sababu ni nyingi sana na zinaweza kutofautiana sana baina ya mtu na mtu.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo katika sehemu ya comment, je ulikua unatumia huduma hii katika kuhakikisha unafuta baadhi ya mafaili katika kifaa chako cha iPhone?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii