fbpx

Chrome, Google Chrome, Jinsi, Maujanja, Teknolojia

Jinsi Ya Ku ‘Lock’ Kivinjari Cha Google Chrome Kwa Kutumia Neno Siri (Password)!

jinsi-ya-ku-lock-kivinjari-cha-google-chrome-kwa-kutumia-neno-siri-password

Sambaza

Ngoja kwanza, hivi umesoma kuhusu Jinsi Ya Ku ‘Lock’ Kivinjari Cha Mozilla Kwa Kutumia Neno Siri (Password)? kama bado Bofya hapa. Kama unavyojua muda mwingine ni vizuri kuweka neno siri katika kivinjari unachotumia.

Hii itakusaidia na kukuhakikishia hata pale unapotoka katika mitandao yako ya kijamii bila ku ‘sign out’ kuwa taarifa zako hazitaishia kwenye mikono mibaya. Hii inamaanisha kuwa mtumiaji wa kivinjari hicho cha Google Chrome itamlazimu aingize neno siri wakati akiwa anafungua kivinjari hicho.

Jinsi Ya Kuloki Google Chrome Kwa Kutumia Neno Siri

Google Chrome inatoa neno siri kwa ajili ya kulinda taarifa za watumaiji wake. Kwa kutumia huduma hii ya usalama utaweza kuloki kivinjari chako cha google tena bila hata ya kukariri neno  siri jipya/lingine kwani utatumia lile la google (lile neno siri moja kwa akaunti zote za Google). Kuweza hili fuata hatua zifuatazo

 • Fungua kivinjari cha Google Chrome na Kisha andika chrome://flags katika sehemu ya kuandika tovuti kisha bofya enter
 • Bofya Ctrl + F kisha andika Enable new profile management system alafu bofya enter
INAYOHUSIANA  Mabetri ya gari la BMW i3 kutumika kwa ajili ya umeme wa majumbani

how-to-lock-chrome-browser-with-a-password

 • Badilisha neno default na kuwa enabled katika machaguo matatu katika kibox
 • Ukiangalia kwa chini utaaona neno Relaunch Now, click hapo
 • ‘Sign in’ katika akaunti yako ya google kwa kubofya kialama kilicho upande wa kushoto kutoka kwa  kialama cha ku ‘minimize’
 • Kisha bofya menu ya Google chrome na kisha nenda katika eneo la ‘settings‘. ukiwa katika settings angalia palipoandikwa ‘People’ na kisha click Add Person

how-to-make-Google-Chrome-password-protected

 • Weka Alama ya tiki kwenye neno ‘Control and view the websites this person visits’ na kisha bofya add
 • Click katika kialama cha akaunti kushoto kwa alama ya ku ‘minimize’, utaona kialama cha kuweka loki. Click sehemu hiyo ya kuweka loki mda wowote unapotaka kukiweka kivinjari chako katika hali ya usalama. Neno siri la kivinjari hiki litakuwa sawa na lile la akaunti yako ya google.
INAYOHUSIANA  NASA, Uber kuleta usafiri wa anga katika miji yenye watu wengi

Je Njia Ya Hapo Juu Imekuchanganya? TeknoKona Inazidi Kukufumbua, Haya Twende Hii Ya Pili Na Rahisi.

Hii ni njia rahisi ya kukifanya kivinjari chako cha  Google Chrome kibaki katika hali ya usalama. Kwa mfano labda ulikuwa unafanya kazi katika kivinjari chako na ukakiacha kwa dakika tano tuu, basi kivinajari kitatoa maombi ya mtu kuingiza neno siri ili kuendelea kukitumia.

 • Fungua WebStore katika kivinjari chako cha google chrome na kisha andika Browser Locker au nenda moja kwa moja kwa kubofya hapa
 • Click ADD TO CHROME  kukiwezesha katika google chrome. Kitatokea kiboxi kikikuuliza kuhakikisha kisha bofya Add
 • Mara tuu baada ya hiyo ‘Browser locker‘ kuingia katika kivinjari chako. Itakuaomba ujaze taarifa zako za neno siri kwa kutengeneza neno siri jipya.
 • Baada ya kuweka neno siri jipya.. kama ukiakaa baada ya muda bila ya kutumia kivinjari chako cha Chrome basi kitaomba uingize neno siri
INAYOHUSIANA  Samsung njiani kufungua viwanda zaidi nchini Marekani

Kama Ukitaka Badilisha Neno Siri Fanya Haya

 1. Nenda katika ‘menu‘ ya chrome kisha eneo la settings
 2. Katika eneo la Settings, click ‘Extensions’ na itaonyesha extentions zote ambazo zimewekwa katika kivinjari hicho
 3. Tafuta Browser Locker na kisha bofya  Options. Itakupeleka katika ukurasa mwingine ambao unaweza weka neno siri jingine/jipya na hata kuseti muda wa kuomba neno siri hilo

Sambaza maujanja haya kwa ndugu na rafiki zako pia.Kumbuka hii itamfaa sana yule ambae anafungua barua pepe, mitandao yake ya kijamii na mengine mengi katika kivinjari kimoja (Google Chrome) na huwa anasahau ku ‘log out’ katika mitandao hiyo. Neno siri litamlindia taarifa zake za muhimu. TeknoKona Tupo Nawe!

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Hashdough

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Reply your comment

Your email address will not be published. Required fields are marked*