Kwa kipindi cha miezi kadhaa wengi wametuomba tuichambue simu ya Tecno Phantom 5, na tukataka tukifanya hivyo basi iwe ni baada ya kuitumia. Ifahamu kwa undani.
Tecno Phantom 5 ni simu nyingine ya kiwango cha juu kutoka kampuni ya Tecno. Simu hii ambayo imeanza kupatikana kuanzia miezi ya tisa na kumi mwaka jana bado ni moja inayoendelea kutangazwa sana na kampuni hiyo hadi mwaka huu.
Je unapata nini pale unapoinunua?
Uwekaji wa simu kwenye boksi pamoja na upangaji wa kisasa bado unaendelezwa na Tecno. Kwenye boksi lake simu hiyo inakuja na ‘cover’ lake, pia earphone pamoja na chaja yake.
Tazama video kutoka akaunti yetu ya YouTube inayokuonesha utakachokutana nacho ukifungua boksi la Tecno Phantom 5 mara baada ya kununua.
Muonekano wa Tecno Phantom 5
Tecno Phantom 5 inakuja na kioo cha ukubwa wa inchi 5.5, kioo kikiwa ni cha teknolojia ya vioo vigumu vya Gorilla Glass toleo la 3. Hii ina maanisha kioo hakitachubuka au kukwanguka kirahisi, ni kigumu kuvunjika pia.
Cha kusifiwa kwa Tecno kwenye Phantom 5 ni pamoja na uamuzi wa kutumia chuma (Metal) katika simu hiyo. Hii inaleta utofauti ikilinganishwa na simu zingine ambazo majumba yake (housing)
Inakuja na kamera mbili, ya selfi ni ya megapixel 8 na inakuja na uwezo wa flash pia, wakati kamera ya nyuma ni ya megapixel 13.
Nyuma pia kuna sensor spesheli ya kusoma alama za vidole – ‘Fingerprint scanner‘. Kupitia hii basi hautaitaji kuingiza nywila (password) kwa kuandika, utaweza fungua simu yako mara moja baada ya kugususha kidole husika kwenye scanner hiyo.
Kwa majaribio niliyoyafanya fingerprint sensor ya Tecno Phantom 5 inafanya kazi kwa haraka sana – hautasubiri.
Pembeni inamaeneo ya kuzima na kuwasha, pa kuongezea sauti na pia sehemu ya kuchomeka memori kadi na pia sehemu ya kuweka laini za simu (mbili).
Kamera yake na Upigaji picha!
Phantom 5 inakuja na kamera yenye kiwango cha juu katika eneo la Megapixels, hii ikiwa ni Megapixel 13 kwa kamera ya nyuma na megapixel 8 kwa kamera ya selfi na hizi zote zikiwa na uwezo wa kutoa mwanga wa ziada (flash).
Ona ubora wa picha zake hapa; (Picha hizi zilipigwa mida ya asubuhi, jijini Dar es salaam)
Tecno Phantom 5: Kiundani
Tazama video ya uchambuzi wa Tecno Phantom 5 kutoka kwenye akaunti yetu ya YouTube.
Laini mbili: Kuna wengi ambao bado wanaona umefikia muda wa Tecno kutoa matoleo ya laini moja pia kwa baadhi ya simu zao za hadhi ya juu kama matoleo ya Phantom. Phantom 5 inakuja na uwezo wa laini mbili, (Micro).
Inatumia Programu endeshaji ya Android, toleo la 5.1 Lollipop… na uchunguzi wa haraka haraka unaonesha kuna uwezekano watumiaji wake wakapata sasisho (update) ya kuwapeleka Android 6.0 – tutachunguza zaidi kuhusu hili, kama ni la kweli basi ni habari njema.
Inakuja na diski uhifadhi wa GB 32, ila utakutana na nafasi ya takribani GB 25 za kutumia. Nafasi ya kutumia memori kadi (Micro SD) kunakupa uwezo wa kuweka kadi ya hadi kufikia GB 128
Inakuja na kiwango cha RAM cha kutosha, hii ikiwa ni cha GB 3 na hii itasaidia kuhakikisha hakuna apps zinazokuwa nzito pale unapoitumia.
Sifa zingine;
- Inakubali hadi teknolojia ya 4G LTE (EDGE, 3G, 4G)
- Display – Inchi 5.5, Pixels 1080 x 1920 (401 PPI), HD, Gorilla Glass 3
- Aina ya prosesa: 64 Bit Octa-core 1.3 GHz CPU (Mediatek MT6753)
- Prosesa ya Graphics – Mali-T720 (Hii itasaidia kufanya ubora wa vitu kama uchezaji magemu uwe mzuri)
- Betri la kutochomoa; mAh 3,000
- Pia teknolojia zingine zote muhimu zinapatikana kama vile Bluetooth, Hotspot (Tethering), WiFi n.k
Mtazamo wa Teknokona
🙂 – Kizuri
i. Tecno Phantom 5 ni toleo jingine linaloonesha ni kwa namna gani kampuni ya Tecno inaonesha uwezo wake katika kutengeneza simu za kisasa na zilizobora. Uwepo wa teknolojia za kisasa kama Fingerprint Sensor pamoja na utumiaji wa ‘housing’ ya mali ghafi (material) ya bati na kuachana na maplastiki ni vitu vinavyoipa Phantom 5 pointi muhimu za ubora. Phantom 5 inamuonekano mzuri.
🙁 – Maoni…..
i. Tunadhani muda umefika kwa Tecno katika baadhi ya simu za hadhi ya juu kama hii kuwe na matoleo ya laini moja pia. Kuna watumiaji ambao huwa hawataki kabisa kununua simu inayotumia laini mbili, kwa sababu zao wenyewe. Ni vizuri kama mnunuaji akiwa anataka toleo la Phantom 5 akutane na chaguo la laini moja au mbili, hili linawezekana.
ii. Kingine kinachoweza kuwa tatizo kidogo ni bei yake, kwa wengi bado bei yake inaweza ikawa ni juu sana ingawa simu inakuja na ubora wa kuvutia na unaolingana na bei kwa kiasi flani…Kizuri gharama! 🙂
No Comment! Be the first one.