fbpx

Halotel Tanzania waboresha kifurushi cha Tomato

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Moja ya siri kuhusu kufanikiwa kwenye biashara yoyote ile ni kuwa mbunifu na Halotel Tanzania wamekuwa wakitoa huduma ambazo zinatokea kupendwa na wateja hiyo kuifanya kampuni husika kuendelea wateja wapya na wa zamani.

Sio mara moja, mbili, tatu tumeshaandika habari kuhusu kampuni inayojishulisha na mawasiliano ya simu wenye ardhi ya Tanzania ambapo tangu kuanzishwa kwake imekuwa ikikuwa mwaka hadi mwaka. Utakumbuka karibu miezi miwili iliyopita Halotel Tanzania walizindua vifurushi vya “Royal” na “Tomato” ilivyolenga kuvutia na kufanya mawasiliano kuwa nafuu zaidi. Kufahamu kwa undani kuhusu vifurushi vya Tomato/Royal BOFYA HAPA.

 

Sasa mwezi Aprili 2019 kampuni hiyo ya mawasiliano nchini Tanzania wameboresha kifurushi cha Tomato kwa kumpa uwanja wa kuongea na mtu kwa njia ya simu bila kukuathiri sekunde izonunua kwa kila dakika tano za mwanzo kwa simu kutoka Halotel kwenda mitandao yote Tanzania.

Kifurushi hicho ambacho kimeboreshwa kinaitwa “TOMATO PLUS”. Baada ya kununua kifurushi hicho mteja ataweza kuongea BURE dakika tano (5) za kwaza bila kujali mtandao husika ambapo haijalishi namba ni ya Vodacom Tanzania, TTCL, Zantel, n.k.

Kuletwa kwa kifurushi cha Tomato kilichoboreshwa kinaweza kuwa msaada kwa wengi hivyo basi wateja wake kupata muda mrefu wa kuongea na ndugu, jamaa na marafiki bila wasiwasi wa kuogopa kuishiwa na salio baada ya muda mfupi. Vipi wewe msomaji wetu, unazungumziaji kuboreshwa kwa kifurushi husika?

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.