Wengi walitegemea mengi baada ya Microsoft kuingia rasmi katika biashara ya utengenezaji na uuzaji wa simu pale waliponunua kitengo cha biashara ya simu kutoka kampuni ya Nokia.
Na sasa miaka kadhaa imepita inaonekana bado kabisa Microsoft hawajafanikiwa kupata maendeleo makubwa ya kimauzo yanayoonesha ukuaji wa biashara hiyo kwao.
Ushindani katika soko la simu janja umekua na taratibu wasioweza kubadilika na kuleta mambo mapya na kujitangaza vizuri yanajikuta yakizidi kupata faida ndogo.
Katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili Microsoft kuzidi kuzitangaza simu za Windows (Windows Phone) bado simu hizo hazijafanikiwa kimauzo.
2013 – Mwaka ambao Microsoft walinunua rasmi kitengo cha biashara ya simu cha Nokia kwa zaidi ya dola bilioni 7.2. Nokia ikabakia na vitengo vyako vingine vyote na kuachia biashara ya simu tuu kwenda Microsoft, hii ikiwa ni pamoja na wafanyakazi na vingine vingi vilivyokuwa chini ya kitengo cha biashara ya simu.
Kutopata faida katika biashara hiyo kuliilazimisha kufanya mabadiliko makubwa kwenye kitengo cha biashara ya simu; hii ilikuwa ni pamoja na kupunguza wafanyakazi wengi na kufanya uamuzi wa kutoa matoleo machache ya simu kwa mwaka na kuachana na utaratibu wa kutoa simu janja za aina mbalimbali ndani ya kipindi kichache.
Microsoft iliachisha kazi zaidi ya wafanyakazi 7800 kutoka kitengo cha simu kama moja ya hatua ya kupunguza hasara kutoka kwenye biashara ya hiyo.
Asilimia ya Mauzo ya Simu janja na Programu Endeshaji Inayotumia
Microsoft wanaamini toleo la Windows 10 na uwepo wa sasa wa simu janja bora zinazotumia toleo hilo pia kwenye simu litasaidia zaidi uuzaji wa simu hizo. Lakini bado kikwazo kikubwa kwao kinaendelea kuwa ni kutokukua kwa haraka kwa soko la apps la simu za Windows.
Hivi karibuni aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Microsoft, Bwana Steve Ballmer, alisema imefikia muda inabidi kuruhusu apps za Android kuweza kupakuliwa katika simu za Windows moja kwa moja bila kizuizi. Steve Ballmer anaamini hiyo ndio njia kuu ya kuweza kuwa na uhakika wa simu za Windows kuweza kufanikiwa kwa haraka zaidi kimauzo. (Chanzo – Digital Trends)
Mafanikio makuwa ya kimauzo kwa simu za Android na za Apple, iPhone, ni pamoja na upatikanaji mkubwa wa apps mbalimbali. Kwa kipindi kirefu Microsoft wameshindwa kuwavutia watengenezaji apps kutengeneza kwa ajili ya simu za Windows, na hii inatokona na mauzo madogo ya simu hizo na hivyo hawaoni faida watakayoipata.
No Comment! Be the first one.